Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camilius Wambura ameipongeza Jumuiya ya Maridhiano na Amani ya Mkoa wa Morogoro huku akiitaka jumuiya hiyo kudumisha Amani iliyopo na kwamba anaamini hilo liko ndani ya uwezo wao kwa sababu asilimia kubwa ya Wajumbe wake ni Viongozi wa Dini.
IGP Wambura ametoa pongezi hizo Oktoba 19 mwaka huu wakati akisalimiana na Wajumbe wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani ya Mkoa wa Morogoro ambao wamekutana na Mkuu wa Mkoa huo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Amani.
Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi Nchini amesema Viongozi wa dini ambao ndiyo wajumbe wa kamati hizo wanamchango mkubwa katika kudumisha amani hapa nchini kupitia mafundisho wanayoyatoa kwa waumini wao, hivyo amesema Serikali inatarajia kuwa amani iliyopo itadumishwa.
“...kikubwa kama tu alivyosema Mkuu wa Mkoa, matarajio yetu na mategemeo yetu kwenu katika suala zima la amani, kudumisha amani kwenye nchi yetu matarajio yetu ni makubwa sana...unaweza ukatumia nguvu kubwa sana na ukakosa uwepo wa amani kwenye Taifa...” amesema IGP Wambura.
Aidha, IGP Wambura amesema Jumuiya ya Maridhiano na Amani ni chanzo muhimu katika upatikanaji wa amani hapa nchini kwa kuwa viongozi hao wanaushawishi mkubwa katika jamii wanamoishi.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.