Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Jaji Ratifa Mansuli amewaasa wajumbe wa kamati ya maadili ya maafisa wa mahakama ya Mkoa huo kufuata miongozo waliopewa, kuzifahamu sheria, kanuni na taratibu za kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya wanamorogoro na Taifa kwa ujumla.
Jaji huyo ametoa ushauri huo wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha wajumbe wa kamati ya maadili ya maafisa wa mahakama wa Mkoa huo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ikiwa na lengo la kusimamia maadili ya mahakimu za Mkoa huo.
“… kabla ya leo tuliwaletea kanuni, z ipo kama mbili za kuonesha jinsi gani ya kuendesha kamati hizi. zile kanuni zimerahisisha kabisa…” amesema Jaji huyo.
Aidha, Jaji Mansuli amesema kamati hiyo yenye wajumbe 7 ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe Adam Kighom Malima ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro imekamilika kisheria baada ya kuapishwa na inatakiwa kuanza majukumu yake mara moja.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wajumbe wenzake amemshukuru Rais kwa uteuzi huo na kumfanya kuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo ambayo ina kazi mahususi ya kulinda amani, ulinzi na usalama katika Mkoa huo.
Amesema, kamati hiyo ya kulinda maadili ndani ya Mkoa huo, itafanya kazi kwa weledi na ufanisi na inakwenda kutoa maamuzi yake bila chuki au kumuonea mtu yeyote ili kila mwananchi wa Morogoro apate haki yake ya msingi.
Mwisho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.