Jamhuri ya Czechslovakia imepanga kuwekeza katika teknolojia mbalimbali hapa nchini hususan Mkoani Morogoro mbapo wanatarajia kuwekeza katika usafiri wa anga kupitia ndege zinazobeba abilia kuanzia wanne.
Hayo yamebainishwa Agosti 15, mwaka huu na Balozi wa Heshima kutoka Jamhuri ya Czech nchini Tanzania Bw. Roman Groling wakati wa mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima ofisini kwake.
Bw. Roman Groling akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Bw. Groling amesema nchi ya Czech kupitia Balozi wa nchi hiyo italeta teknolojia ya utengenezaji wa ndege ndogo zinazobeba abilia kuanzia wawili hadi wanne, amesema teknolojia hiyo itazinduliwa Mkoani Morogoro.
Aidha, Bw. Groling ameongeza kuwa teknolojia hiyo itahusisha utengenezaji wa ndege zisizo na rubani (drones), pamoja na uwekezaji wa usafiri wa maroli ya kisasa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima akipokea zawadi kutoka kwa Bw. Roman Groling.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amemshukuru Rais Samia kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ambapo ujio wa wawekezaji hapa nchini ni jitihada za Rais Samia.
Ameongeza kuwa uwekezaji huo ni fursa kwa Mkoa wa Morogoro, hivyo amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani na utulivu ili kuwavutia wawekezaji wengi na kufanya uchumi wa nchi kukua.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Heshima Bw. Roman Groling baada ya mazungumzo Yao.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.