• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

KAMISHNA MSAIDIZI MKOA WA MOROGORO AELEKEZA WANANCHI NA VIONGOZI WA VIJIJI KUTOUZA KIHOLELA ARDHI ZA VIJIJI.

Posted on: October 7th, 2024



Watendaji wa Vijiji, Vitongoji, Wenyeviti, na Wajumbe wa mabaraza ya Serikali za Vijiji wametakiwa kuacha tabia ya kuuza maeneo kiholela kwa wananchi, ili kuepusha migogoro inayochafua sifa ya Serikali.

Rai hiyo imetolewa Oktoba 5, 2024 na Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Mkoa wa Morogoro Bw. Idrisa Kayera, alipofika kwenye mashamba ya wakulima waliodai kununua maeneo ndani ya sehemu zilizotengwa kwa ajili ya akiba na malisho ya mifugo katika Vijiji vya Msolwa, Kalengakelo, na Chisano.

Mmoja wa wanakijiji anayefahamika kwa jina la Utaisoma, alieleza kuwa shamba alilonunua kutoka kwa uongozi wa kijiji limeingizwa kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi na kuwekwa kama eneo la malisho, jambo lililopunguza uzalishaji wake.

Utaisoma alimlaumu uongozi wa kata na kijiji, akidai kuwa amemiliki maeneo hayo kwa zaidi ya miaka 16 bila kuwa na vielelezo halali vya umiliki wa ardhi hiyo.

Akijibu malalamiko hayo, Diwani wa Kata ya Kalengakelo  Martha Mkula, alisema maeneo hayo yaliuzwa na uongozi wa kijiji uliomaliza muda wake mwaka 2014 ambapo mtendaji wa kijiji alihusika katika mchakato huo.

Martha aliongeza kuwa baada ya kutenga maeneo ya malisho, waligundua kuwa mkulima mmoja amelima katikati ya eneo hilo la malisho. Alipomhoji mwenyekiti wa kijiji, alikiri kupokea shilingi milioni moja kutoka kwa Utaisoma kama malipo ya shamba hilo.

“..Nikamwambia mwenyekiti, huoni kuwa unaleta mgogoro hapa? Tumekubaliana kuwa eneo hili ni kwa ajili ya malisho, lakini wewe na vijana wako mnaenda kuuzia wakulima. Nakushauri urudishe fedha hizo, lakini hakunisikiliza. Kama angefuata ushauri wangu, tusingekuwa hapa leo.." alisema Martha.

Naye Leonard Kifanyi, mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Kalengakelo, aliongeza kuwa maeneo hayo awali yalikuwa chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori (TAWA) kabla ya kurejeshwa kwa kijiji, hivyo wakapanga matumizi bora ya ardhi kwa kuyagawa kwa wakulima na wafugaji.

Licha ya mipango hiyo, baadhi ya wananchi walivamia maeneo ya malisho na kuanza shughuli za kilimo, jambo ambalo liliendelea kuzua migogoro, alisema Kifanyi.

Baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi na majibu ya viongozi, Kamishna Kayera aliagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili viongozi waliotajwa na kuwachukulia hatua za kisheria iwapo watabaini ukweli.

Aidha, Kamishna Kayera alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kujua taratibu sahihi za kufuata anapotaka kununua ardhi, huku akiwataka viongozi wa vijiji kuacha tabia ya kuuza maeneo kana kwamba ni mali yao binafsi.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.