• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Kampeni ya Mama Samia kuwa mwarobaini wa Migogoro ya wakulima na wafugaji Kilosa.

Posted on: December 15th, 2024

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Wilaya ya Kilosa imekuwa ikikabiliwa na migogoro mingi ikiwemo ya wakulima na wafugaji na kwamba imekuwa makao makuu ya migogoro ambayo mwarobaini wake ni Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia - Mama Samia legal Aid Campaign.

Waziri Ndumbaro amebainisha hayo Disemba 15, Mwaka huu wakati akizindua kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika kata ya Magomeni Wilayani Kilosa Mkoani humo ikiwa ni siku ya pili baada ya kampeni hiyo kuzinduliwa Kimkoa Disemba 13, 2024.

Akifafanua zaidi, Waziri huyo amesema migogoro inayowakabili wananchi wa Kilosa kumeifanya Wizara ya Uvuvi na Mifugo kuteua Kilosa kuwa makao makuu ya migogoro ya wakulima na wafugaji, hivyo ameitaka timu ya wanasheria wa kampeni hiyo kuandaa ripoti itakayoonesha migogoro iliyotatuliwa na ambayo haijatatuliwa ili ambayo haijatatuliwa ifanyiwe oparesheni maalum ya siku kumi kuhakikisha inaisha.

"...Na mimi niseme sasa baada ya siku hizi kumi itaandaliwa ripoti yenye kuainisha migogoro ipi imekwisha na ipi imesalia ile ambayo imesalia tutakuja na operesheni maalum kumaliza migogoro hiyo..." Amesema Mhe.Damas Ndumbaro

Sambamba na hayo, amewataka wananchi wa Mkoa wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni hiyo mara itakapofika katika maeneo yao kwa lengo la kupata usaidizi wa kisheria ili kusuruhisha migogoro yao kwa kufuata misingi ya sheria ili haki ipatikane bila kumuonea mwingine.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemuomba Waziri wa Katiba na Sheria kuongezewa muda wa kampeni hiyo kwani amesema Wilaya hiyo ni kubwa ambapo Kata 10 na Vijiji 30 pekee vilivyobainishwa kufanyika kampeni hiyo haitakidhi haja ya wananchi wengi wa Wilaya hiyo kufikiwa na Kampeni hiyo.

Amesema, Wilaya hiyo inakabiliwa na migogoro mingi hususan ya wakulima na Wafugaji, migogoro ya kijamii ikiwemo ukatili wa jinsia ya wanawake na watoto, mirathi na ardhi, hivyo kufika kwa msaada huo wa kisheria Kutatatua kero nyingi za kijamii Wilayani na Mkoa kwa ujumla.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Kilosa ambaye pia ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kutumia ujio wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kupata ufumbuzi wa migogoro yao.

Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.