Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro inapenda kuwataarifu wananchi wa Mkoa huo kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 zitafanyika kuanzia Aprili 20 hadi Aprili 30, 2024. Wananchi wote mnaombwa kuupokea mwenge huo katika maeneo yote utakapopita na kuushangilia pia kukesha nao kwa kuwa lengo la kukimbiza mwenge wa uhuru ni kuleta maendeleo mbalimbali katika maeneo yetu.
Kaulimbiu ya mwenge wa Uhuru mwaka huu ni TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, KWA UJENZI WA TAIFA ENDELEVU. Mwenge huo utapokelewa katika Wilaya ya Mvomero ukitokea Mkoa wa Tanga, siku ya Jumamosi 20/4/2024
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.