• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

KASI YA MAENDELEO NI KUBWA REA NA TANESCO FANYENI KAZI - DKT. BITEKO

Posted on: May 31st, 2024


KASI YA MAENDELEO NI KUBWA REA NA TANESCO FANYENI KAZI - DKT. BITEKO.

Naibu Waziri Mkuu ambae pia ni Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (MB) amezitaka Mamlaka ya Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA) na Shirika la Usamabazaji wa Umeme Tanzania (TANESCO) kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuendana uhalisia wa uhitaji wa nishati ya umeme na kasi ya maendeleo hapa nchini.
Dkt. Doto Biteko amesema hayo Mei 31, 2024 wakati akifungua rasmi kituo cha kupoza umeme cha Ifakara Mji kilichopo  Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro  huku akibainisha kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha  shilingi Bilioni 24.59 huku  shilingi bilioni 18 ni ufadhili wa jumuiya ya Ulaya kupitia mfuko wa maendeleo wa umoja wa Jumuiya ya Ulaya ( European Development Fund EDF).

".... TANESCO na REA endeleeni kuwahudumia wananchi kwa sababu kasi ya maendeleo ni kubwa sana .." amesema Dkt. Biteko.

Aidha Dkt. Biteko amesema mradi huo utaenda kuongeza thamani ya mazao yanayochakatwa kupitia viwanda kama mchele huku wakitarajia kufungua viwanda 54 vitakavyotumia umeme na pia umeme huo utatumika mashuleni ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.


Hata hivyo Dkt. Biteko amesema kuna uhitaji wa kufungua Ofisi ndogo katika  maeneo ya karibu na kituo hicho ili kuweza kusogeza zaidi huduma hiyo kwa wananchi huku akiwapongeza wakandarasi waliotekeleza ujenzi wa kituo hicho akisema wamefanya kazi nzuri na kuutendea haki mradi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema Mkoa wa Morogoro ndio Mkoa unaongoza kwa uzalishaji wa sukari Nchini hivyo kupitia mradi huo utakwenda kupunguza  adha ya upatikanaji wa nishati hiyo  na kuvisaidia viwanda vidogo vidogo ambavyo vilikuwa havifanyi kazi sababu ya ukosefu wa umeme wa kutosha kuweza kufanya kazi.


Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema Mkoa wa Morogoro kupitia uwekezaji wa kituo hicho utaenda kuwavutia wawekezaji mbalimbali kwenda kuwekeza Mkoani humo kutokana na upatikanaji wa uhakika wa nishati hiyo ya umeme ukiwemo uwekezaji kupitia uchimbaji wa madini aina ya graphite yanayopatikana Wilaya ya Ulanga.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amemuhakikishia Naibu Waziri Mkuu huyo kuwa watatunza vyanzo vya maji  maeneo ya hifadhi na kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa wale wote wanaoharibu vyanzo vya maji kwa makusudi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini Mstaafu Meja Jenerali Dkt. Jacob Kingu amesema Bodi ya nishati vijijini kwa kushirikiana na  Menejimenti ya wakala wa nishati vijijini itaendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara na Nishati na kuhakikisha nishati ya umeme nchini inapatikana katika maeneo yote ya vijijini.

Nao wananchi akiwemo  Ali Mohamed mkazi wa Kijiji cha Kibaoni kwa niaba ya wananchi wenzake ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mradi huo wa kupoza umeme na kwamba utapunguza changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara ambapo wataanza kufanya biashara zao za kutumia umeme bila usumbufu.


Ujenzi wa mradi huo ulianza Machi 24, 2020 na kukamilika Machi 31 mwaka huu kwamba mradi huo  utazinufaisha Wilaya tatu za Ulanga, Malinyi na Kilombero na kuondoa changamoto ya umeme    na kuongeza kasi ya maendeleo ya wananchi wa Wilaya hizo kupitia usindikaji wa mazao ya kilimo, uchimbaji wa madini na kuimarisha huduma za kijamiii.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.