Katibu Mkuu OR - TAMISEMI atembelea ujenzi Ofisi ya RC Morogoro
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe ametembelea ujenzi wa jengo la Ofisi mpya ya Mkuu wa MKoa wa Morogoro na kupongeza kazi inayoendelea huku akimuagiza Mkandarasi wa kazi hiyo kuongeza kasi ili kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati.
Mhandisi anayesimamia ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (Mhandisi Queen Sanga).
Prof. Shemdoe ametoa maagizo hayo Oktoba 8 Mwaka huu baada ya kutembelea eneo la ujenzi ambalo lipo pembeni kidogo mwa Ofisi ya sasa ya Mkuu wa Mkoa huo kwa lengo la kuona hatua Ujenzi iliyofikiwa baada ya Serikali kutoa fedha zaidi ya shilingi Bil.6 kujenga Ofisi hiyo.
Akiwa katika eneo la Mradi, Katibu Mkuu Prof. Shemdoe alipongeza juhudi zinazoendelea za ujenzi huo hata hivyo alimtaka Mkandarasi wa Jengo hilo lenye Ghorofa Moja kuongeza kasi na kukamilisha kazi hiyo kama Mkataba unavyoonesha.
“Nimefika kutembelea na kuona maendeleo ya kazi za Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa MKoa, kazi imeanza vizuri, ongezeni juhudi ili tuwe sawa na Mpango” ameagiza Katibu Mkuu.
Mojawapo ya majengo ya sasa yanayotumika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Prof. Shemdoe ni muumini wa kusimamia kwa vitendo fedha zote za Serikali zinazopita katika Ofisi yake, Lengo ni kutaka miradi inayotekelezwa iwe na ubora unaofanana na fedha zilizotolewa na serikali (Value for Money) ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Muonekano wa Jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa litakapokamilika.
Kwa upande wake Mhandasi Queen Sanga anayesimamia Ujenzi huo kwa niaba ya Kampuni ya MCB Ltd kutoka Mbeya amesema kwa mujibu wa Mkataba wa ujenzi huo wako nyuma kidogo kutokana na sababu za kiufundi, hata hiyvo amesema wana mpango kabambe wa kufanya kazi ya ujenzi usiku na mchana ili kufidia gape lililopo hivyo kuwa sawa na Mkataba unavyoeleza.
Katibu Mkuu, OR- TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe (kulia) akitoa maelekezo ya kiutendaji kwa Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Mhandisi Ezron Kilamhama.
Naye Msimamizi wa Ujenzi huo Mhandisi Ezron Kilamhama ambaye Pia ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Miundombinu Mkoa wa Morogoro amesema, ujio wa Katibu Mkuu OR - TAMISEMI kufika eneo la mradi, kupongeza na kutoa maelekezo ya namna ya kuleta ufanisi wa ujenzi huo kumempa nguvu zaidi ya kusimamia mradi huo.
Katibu Mkuu OR- TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe akisaini kitabu Cha wageni alipotembelea site hiyo.
Ujenzi wa jengo la Ofisi Mpya ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa mujibu wa Mkataba ni wa kipindi cha miaka miwili (2) kuanzia 27 May 2022 hadi 26 May 2024 na utakagharimu shilingi za kitanzania 6,597,777,757,.90
Ujenzi wa Ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ukiendelea.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.