• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

KATIBU TAWALA MKOA WA MOROGORO ATOA WITO KWA WADAU.

Posted on: May 24th, 2022

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Mtunguja amewaasa wadau wa Lishe Mkoani humo kuunganisha nguvu zao na kuona njia bora ya kukwamua hali duni ya lishe kwa watoto walio chini ya miaka mitano baada ya takwimu kuonesha kuwa zaidi ya asilimia 43% ya Watoto wa umri huo hapa nchini kuwa na udumavu ukiwemo Mkoa wa Morogoro ambao unazalisha vyakula vya kila aina.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bi. marim Mtunguja akifungua Kikao cha programu jumuishi ya Taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto  kilichofanyika katika Ukumbi Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mei 23 Mwaka huu.


Hayo yamebainishwa Mei 23 Mwaka huu wakati wa Kikao cha ufunguzi wa Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi na makuzi ya awali ya mtoto kupitia Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Mariam Mtunguja, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.




Katibu Tawala huyo amesema pamoja na kuwa Mkoa wetu haupo ndani ya orodha ya mikoa kumi yenye idadi kubwa ya watoto waliodumaa inasikitisha kuwa bado Mkoa wa Morogoro unatajwa kuwa na hali ya lishe isiyoridhisha hali ywa kua Mkoa wetu kuwa na bahati ya kuzalisha vyakula vya aina mbalimbali.





“Na inasikitisha zaidi kwamba tunazalisha chakula kwa wnigi ikiwemo Mahindi, Mpunga, Matunda na Mbogamboga kila kitu tunacho lakini hali ya udumavu wa watoto wetu ni kubwa” amesema Bi. Mariam Mtunguja.




Aidha, Katibu Tawala huyo wa Mkoa, amebainisha changamoto zinazoweza kukabili maendeleo ya ukuaji wa watoto chini ya umri huo ambapo ili mzazi au mlezi aweze kubaini changamoto hizo, mzazi au mlezi huyo anapaswa kuwa karibu zaidi na mtoto kwa kipindi chote cha hatua za ukuaji wake.

“Asilimia 43% ya watoto wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua timilifu na maendeleo ya ukuaji wao, kwa kusababisha na utapiamlo, kukosekana kwa uhakika wa chakula, miundombinu katika familia msongo wa mawazo, uhaba wa rasilimali pamoja na unyanyasaji wa watoto” amesema Bi. Mariam Mtunguja.




Katika hatua nyingine, Katibu Tawala huyo wa Mkoa kupitia hotuba hiyo ameweka wazi kuwa, maendeleo katika ukuaji wa mtoto ni matokeo ya Afua mbalimbali zinazohusisha wadau wa Sekta tofauti ambazo zina wajibika kutoa afua hizo kwa kuzingatia hali halisi ya huduma za malezi jumuishi kwa watoto wadogo kwa kutumia mifumo ya usimamizi na uratibu wa utoaji wa huduma hizo hapa nchini.





Kwa upande wake Bi. Germana Mung’aho ambaye ni Afisa elimu wa Mkoa wa Morogoro amekemea baadhi ya walimu wanaowafanyia ukatili wanafunzi wa madarasa ya awali kwa kuwaadhibu inapotokea wamechelewa kufika shuleni na kutumia vyumba vyenye hali isiyoridhisha katika kuwafundisha, kwani kufanya hivyo kwa watoto hao ni kuchangia kuwadumaza kiakili na kimwili kwa kuwasababishia msongo wa mawazo na ulemavu kwa ujumla.



Bi. Germana Mung’aho ambaye ni Afisa elimu wa Mkoa wa Morogoro akichangia mada wakati wa   ufunguzi wa Kikao na mafunzo ya programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kilichofanyika katika Ukumbi Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mei 23 Mwaka huu.


Akiwakilisha Wakurugenzi watendaji wa Mkoa huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Bi. Rehema Bwasi amebainisha kuwa kama watendaji watasimamia vema utekelezaji wa Progamu hiyo kwani malezi shirikishi na jumuishi katika makuzi ya watoto ni kitu cha muhimu katika kuwajengea uelewa wa kiakili na kimwili maishani mwao.



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro  Bi. Rehema Bwasi akiwa  wakati wa   ufunguzi wa Kikao na mafunzo ya programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kilichofanyika katika Ukumbi Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mei 23 Mwaka huu.


Naye, Afisa Programu wa Shirika binafsi la CHILDHOOD DEVELOPMENT ORGANISATION (CDO) ambalo ni watekelezaji wenza wa Programu hiyo Jumuishi Bw. Innocent Rusomyo ameweka wazi kwamba. Katika kutekeleza Programu hiyo wameanzisha na kutekeleza miradi kadhaa ya kuboresha elimu ya awali ya watoto katika kusaidia makuzi na malezi bora ya watoto ikiwemo mradi “MTOTO WETU TUNU YETU” ambao unatekelezwa katika Halmashauri tatu za Mlimba, Mvomero na Ifakara Mji.


Afisa Programu wa Shirika binafsi la CHILDHOOD DEVELOPMENT ORGANISATION (CDO) Bw. Innocent Rusomyo akiwa katika ufunguzi wa Kikao cha programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto  kilichofanyika katika Ukumbi Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mei 23 Mwaka huu.




MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.