Mwanamasumbwi maarufu Mkoani Morogoro Twaha Ramadhan almaarufu kama Twaha Kiduku amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela kwa kutambua na kuthamini vipaji vya wanamichezo wa Mkoa wa Morogoro hususan vijana wanaochipukia kwenye tasnia mbalimbali za michezo Mkoani humo.
Twaha Kiduku akipokea cheti cha nidhamu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela.
Twaha Kiduku ametoa kauli hiyo Septemba 11 mwaka huu kwenye hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili yake kumpongeza baada ya ushindi wa pambano lake dhidi ya Abdallah Pazi almaarufu kama Dulla Mbabe iliyofanyika Cate Hoteli iliyopo Halmashauri ya Manispaa Morogoro Mkoani humo.
Twaha Kiduku ametoa shukurani na pongezi kwa Viongozi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya na Mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa huo Martine Shigela, Mkuu wa Wilaya hiyo Albert Msando, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhe. Paschal Kihanga pamoja na wadau mbalimbali wa michezo ya ngumi Mkoani humo hii ikiwa ni baada ya kushinda shindano kati yake na Dulla Mbabe lililofanyika Agosti 20 Jijini Dar es Salaam.
“….Mimi nawaahidi ndugu zangu, mechi zozote ambazo nitaletewa kwa sababu mimi huwa siogopi bondia yoyote, mtu yeyote nikiletewa wewe weka mzigo tupigane show show ….” amesema kiduku.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela ikiwa ni ishara ya mchango wake kwa Mwanamasumbwi Kiduku.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa Morogoro Mhe. Paschal Kihanga akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni ishara ya mchango kwa Mwanamasumbwi huyo.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakipokea vyeti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela ikiwa ni ishara ya mchango wake kwa Mwanamasumbwi Kiduku.
Baadhi ya Wadau wa Mchezo wa ngumi Mkoa wa Morogoro wakipokea vyeti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela ikiwa ni ishara ya mchango wao kwa Mwanamasumbwi Kiduku.
Hafla hiyo iliyoandaliwa na wadau hao wa Michezo Mkoani Morogoro wakishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ililenga pamoja na kumpongeza Mwanamasumbwi Twaha Kiduku lakini pia inakusudia kuwa mikakati mathubuti ya kuwaendeleza wanamasumbwi wote walioko ndani ya Mkoa huo akiwemo Twaha Kiduku.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.