KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AWAASA WANAMOROGORO KUTUNZA MAZINGIRA.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2024 Godfrey Mnzava amewataka wananchi wa Mkoa huo kutunza mazingira ili kuepukana na athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia ya Nchi.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge Kitaifa ametoa wito huo Aprili 20, 2024 siku ya kwanza tu baada ya mbio za Mwenge huo kuanza kukimbizwa Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wakati wa kuona mradi wa utunzaji wa Mazingira (ECO) school unaotekelezwa na shule ya msingi Manyinga iliyopo Wilaya humo.
Ndg. Mnzava amesema kama yalivyomataifa mengine yanapitia katika changamoto ya uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji ama miti, kuchoma mkaa, shughuli za viwanda amabavyo havizingatii utunzaji wa mazingira, kilimo kisichozingatia taratibu na shughuli za ufugaji holela ambapo kupelekea mabadiliko ya tabia ya nchi.
"Lipo jukumu kubwa sana na umuhimu mkubwa sana wa kuendelea kuhakikisha kwamba tunatunza mazingira yetu ili yaweze kutufaidiaha sisi wenyewe Sisi na vizazi vijavyo" amesema kiongozi huyo.
Kwa upande wake Jenifa Solomoni Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Manyinga akiwa ni balozi wa mradi wa utunzaji wa Mazingira (ECO school) amesema kupitia mradi huo, wanatoa elimu katika jamii hasa elimu ya uchumi mzunguko.
Mwenge wa uhuru kesho Aprili 21, 2024 utaendelea kukimbizwa katika Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro ikiwa ni siku yake ya pili tangu kukabidhiwa ukitokea Mkoa wa Tanga.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.