Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru awataka watanzania kuipongeza Serikali
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi amesema kuna kila sababu kwa watanzania kuishukuru Serikali yao na kuipongeza kwa namna inavyojali wananchi wake katika kuwapatia huduma muhimu kama Elimu, Afya na Maji.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Josephine Mwambashi
Luteni Mwambashi amesema hayo wakati wa Mwenge wa Uhuru ukipitia miradi ya maendeleo Wilayani Gairo ambapo pamoja na miradi mingine Mwenge wa uhuru uliona mradi wa maji wa Gairo ambao unagharimu zaidi ya Tsh 2 Bil.
“tuipongeze Serikali yetu kuona umuhim mkubwa kwa sisi wananchi kupata huduma hii ya maji kama ilivyosomwa katika taarifa kuwa huduma ya maji ilikuwa ni shida sana katika Wilaya hii ya Gairo” amesema.
Amesema kutokana na umuhimu wa maji Serikali ya awamu ya sita imesimamia mradi huo na kuona unakamilika kwa lengo la kuwaondolea kero wananchi wa Gairo hivyo hawana budi kuishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakimbiza Mwenge kitaifa wakiwa juu ya tenki la maji kuhakiki utekelezaji wa mradi
Mtambo wa kuchuja maji ya chumvi katika mradi wa maji Gairo
Hata hivyo Luteni Mwambashi amepongeza mradi huo mkubwa unaotumia mtambo wa kisasa katika kuchunja kiwango kikubwa cha chumvi kinachofikia Micro siemens 6000 iliyoko kwenye maji hayo kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA na kufanya maji hayo kuwa safi na salama kwa kunywa.
Katika hatua nyingine Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021 amewataka wananchi pamoja na kutunza vyanzo vya maji lakini pia wanatakiwa kuwa walinzi wa miundombinu ya maji ili isiharibiwe na wapinga maendeleo hivyo kuendelea kupata maji karibu jambo litakalosaidia kupata muda wa kutosha kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabil Makame kwa niaba ya wananchi wa Gairo ameishukuru Serikali kukamilisha mradi huo na kuweka mtambo wa kuchuja maji huku akiahidi kuungana na wananchi wake katika kutunza vyanzo vya maji pamoja na miundombinu yake.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabil Makame akipokea Mwenge wa Uhuru
Mwenge wa uhuru pamoja na miradi mingine sita umepitia mradi huo kwa lengo la kujionea namna unavyotumia TEHAMA katika kuchuja chumvi iliyoko kwenye maji yanayozalishwa hapo uku kiongozi wa mbio za Mwenge akikiri kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.
Mwenge wa Uhuru umekamilisha mbio zake Wilayani Gairo hii leo Agosti 9, 2021 na Agosti 10 utakimbizwa Wilaya ya Morogoro ikikamilisha idadi ya Wilaya saba za Mkoa wa Morogoro na Agosti 11 Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuanza kukimbizwa Mkoani Pwani.
Wakimbiza Mwenge kitaifa wakiwa katika picha ya pamoja na Bahati Msuliche wa Gairo (Mwenye ulemavu wa mikono) baada ya kumwona akiwa katika shughuli za mwenge kwa muda mrefu na mwenge kumzawadia fedha Tsh. 60,000/=
Baadhi ya Wakimbiza mwenge kimkoa wakiteta jambo. kushoto ni Wnnifrida Madeba Mratibu wa mbio za Mwenge kimkoa - Morogoro
Baadhi ya wananfunzi wa shule za Msingi ambao wapo kwenye club za kupinga masuala ya Rushwa
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.