Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa akigawa tuzo mbalimbali na kukagua kitalu cha kutunzia miti na kupanda miti katika shule ya sekondari ya Mazinyungu Wilayani Kilosa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Ndg. Abdallah Shaib akitoa zawadi ya vyeti kwa washindi wa Insha za utunzaji mazingira.
Kiongozi huyo wa mbio za mwenge katika salam zake kwa wakazi wa eneo hilo na watanzania kwa jumla aliwasihi kila mtanzania kupanda miti na kutunza ili kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo vya maji.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ameongoza zoezi la upandaji miti katika shule ya Sekondari Mazinyungu.
Mwenge wa Uhuru leo 10/05/2023 uko Wilayani Kilosa ambapo umepitia Miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya Tsh bilioni 1.2 na kesho utakimbizwa katika Wilaya ya Gairo.
MWISHO
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.