KUSAJIRI BIASHARA LAZIMA UWE NA ANWANI YA MAKAZI
Naibu waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea Mathew amesema hatua inayofuata sasa kuhusu anwani za makazi na Posti Kodi ni kwamba kila mwananchi anatakiwa kuwa na anwani za makazi na kwa wafanyabiashara hicho kitakuwa ni moja ya vigezo muhimu katika kutoa leseni zao za biashara.
“Wafanya biashara wote watakapokwenda kuomba leseni ya kufanya biashara, ni lazima atoa anwani yake ya makazi, asipokuwa na anwani ya makazi hataweza kusajiliwa biashara yake” amesema Naibu Waziri Kundo.
Waziri Kundo amesema hayo Mei 18 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa uwekaji wa vibao vya anwani za makazi katika Kata ya Kichangani Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mkoani humo alipofanya ziara ya siku moja.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea Mathew (kulia) akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela alipofanya ziara ya siku moja Mkoani humo Mei 18 mwaka huu
Naibu Waziri Mhandisi Kundo akiongea na baadhi ya viongozi wa Serikali katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro mara alipowasili kwa zaiara ya siku moja Mei 18 mwaka huu
Naibu Waziri akizindua rasmi uwekaji wa vibao vya anwani za makazi katika moja ya makazi ya mwananchi katika kata ya kichangani Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando akishiriki uwekaji wa vibao vya anwani za Makazi - Kata ya Kichangani
Kulia kwa Naibu Waziri ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga
Katibu Mwenezi wa CCM Tawi la Elia Six Kata ya Kichangani Michael Samweli Kilumbo akishiriki kuweka kibao cha Anwani za Makazi huku akisaidiwa na Naibu Waziri Mhandisi Kundo Mathew
Naibu Waziri Mhandisi Kundo Andrea (mwenye suti) akitoa elimu ya faida ya anwani za Makazi kwa wakazi wa Mkoa huo. kushoto aliyevaa miwani ni Mratibu wa zoezi hilo Mkoa wa Morogoro Mhandisi Ezron Kilamhama
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.