Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani 2023 amabapo kitaifa Maadhimisho hayo yatafanyika Mkoani Morogoro huku Tarehe 24/11/2023 ni ufunguzi rasmi wa Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani 2023 na kufikia kilelel tarehe 01 Disemba, 2023.
Hayo yamebainishawa Novemba 23 mwaka huun na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam kighoma Malima wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Waadishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo uliolenga kutoa taarifa kuhusu Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani 2023 yatakayofanyika Mkoani humo.
Mhe. Malima amesema Wiki ya maadhimishoya siku ya UKIMWI Duniani itazinduliwa tarehe 24 Novemba, 2023 na kufikia kilele tarehe 01 Disemba, 2023. Katika wiki ya kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba kutakuwa na mfululizo wa matukio na utoaji wa huduma mbalimbali zitakazotolewa na wataalamu zikiwemo upimaji wa VVU, uchunguzi wa magonjwa sugu yasiyoambukiza (Kisukari, Shinikizo la damu, uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa kizazi, lishe), elimu na uchunguzi wa Kifua Kikuu, uchangiaji damu na huduma ya kwanza.
“...Katika wiki ya kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba kutakuwa na mfululizo wa matukio na utoaji wa huduma mbalimbali zitakazotolewa na wataalamu zikiwemo upimaji wa VVU, uchunguzi wa magonjwa sugu yasiyoambukiza (Kisukari, Shinikizo la damu, Uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa kizazi, lishe), elimu na uchunguzi wa Kifua Kikuu, uchangiaji damu na huduma ya kwanza...” amesema Mkuu wa Mkoa.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha matukio yatakayofanyika ndani ya Wiki ya Maadhimisho kuwa ni pamoja na Mbio za nyika (ATF Marathon). Amesema Mbio hizo zinalenga kuhamasisha na kuutangaza mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF).
Matukio mengine ni kufanyika kwa Kongamano la Vijana, kongamano la Kitaifa la Kisayansi (National HIV & AIDS Scientific Symposium),Mdahalo wa Viongozi wa Kijamii, tukio la Kilele cha Kijiji cha Vijana pamoja na Mkutano Maalumu wa Wadau wa Udhibiti UKIMWI (High level Partner’s meeting).
Sambamba na hilo Mhe. Adam Malima ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa huo, taasisi zote za Umma na Binafsi, Taasisi za Elimu ya vyuo vikuu na Jumuiya mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye maadhimisho hayo kuanzia siku ya ufunguzi tarehe 24 Novemba, 2023 hadi Disemba Mosi, 2023.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu waishio na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) Bw. Emanuel Msinga ameishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fursa kwa jamii hususan kwa watu waishio na VVU kuonesha mchango wao katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. Aidha, ameishukuru Serikali kwa kutoa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI (ARV).
Mgeni rasmi siku ya kilele cha Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MWISHO.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.