• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yapamba Moto.

Posted on: November 15th, 2023


Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani 2023 ambayo Kitaifa yatafanyika Mkoani Morogoro yamepamba moto ambapo uzinduzi rasmi unategemea kufanyika Novemba 24 huku Mgeni rasmi wa uzinduzi huo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kujadiliana na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Kighoma Malima juu ya kufanisha sherehe ya Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani 2023 ambayo kitaifa itafanyika Mkoani Morogoro.

Hayo yamebainishwa Novemba 15, 2023 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akiwa mkoani Morogoro na kukutana na Mhe. Adam Kighoma Malima na kujadiliana nae mambo kadha wa kadha kuhusu kufanikisha tukio hilo muhim.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Adam Kighoma Malima akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakijadiliana kuhusu kufanikisha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani 2023 ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani Morogoro.

Katika mazungumzo yao, Waziri Mhagama amesema, Maadhimisho hayo yanaenda sambamba na wiki ya maadhimisho ambayo itazinduliwa Novemba 24 na Mkuu wa Mkoa huo ambapo kutakuwa na makongamano ya Vijana, mijadala ya Viongozi wa dini, riadha na maonesho ya wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

Pamoja na maandalizi hayo Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kupima Afya zao kwa hiari na kuchukua taadhari ya maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima ameishukuru Serikali kwa kuupa heshima Mkoa huo kuwa mwenyeji wa Maadhimishao hayo kitaifa na kuahidi kusimamia kwa karibu maandalizi yake hususan ya ngazi ya Mkoa ili sherehe hiyo iwe na mafanikio na matokeo lengwa.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Adam Kighoma Malima, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakiwa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Maadhimisho ya  Siku ya UKIMWI Duniani 2023 ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani Morogoro wakikagua uwanja wa Shule ya Sekondari Morogoro ambao utatumika wakati wa Maadhimisho hayo.

Aidha, amepongeza nia ya Serikali ya kufikisha ujumbe kwa vijana kuhusu kujikinga na maambukizi ya VVU na UKIMWI ambapo utafiti unaonesha kuwa Vijana wapo kwenye hatari ya maambukizi hayo.

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani 2023 yanaenda sambamba na kaulimbiu inayosema “Jamii iongoze kutokomeza UKIMWI”.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.