RC Shigela awabeba wanawake Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amewatetea wanawake Mkoani humo na kutaka wapewe kipaumbele katika harakati zao za kujipatia kipato pamoja na kupinga ukatili na unyanyasaji wa kingono.
Martne Shigela amesema hayo wakati akitoa hotuba yake kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka ambapo kwa Mkoa wa Morogoro maadhimkisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Jamhuri uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Akibainisha hayo Mkuu huyo wa Mkoa amesema, ili mwanamke aweze kuendelea kiuchumi na kuendeleza familia yake na jamii nzima ujumla ni lazima apewe kipaumbele ili aweze kufikia malengo ambapo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ameuagiza uongozi kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wanawake kufanyia biashara zao.
Katika hatua nyingine Martine Shigela ameweka bayana kuwa bado kuna ukatili na unyanyasaji kwa wanawake miongoni mwa jamaii ubaguzi wa kijinsia, uonevu, umiliki wa ardhi na migogoro ya mirathi mambo ambayo amesema hataki kuyasikia ndani ya Mkoa huo na kuagiza vyombo vya sheria kuwashughulikia kwa mujibu wa sharia wale wote ambao wanaendeleza tamaduni hizo.
Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani mwaka huu yalikuwa na kaulimbiu isemayo Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo endelevu.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.