Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amewataka Maafisa Habari kujitokeza hadharani kujibu na kutoa ufafanuzi sahihi kuhusu maendeleo yanayofanywa na Serikali, hususan pale ambapo upotoshaji wa makusudi unapotokea.
Akifungua kikao kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa, Halmashauri, na Taasisi za Ofisi ya Rais - TAMISEMI kilichofanyika Dodoma Mei 23, 2025, Mchengerwa aliwakumbusha wajibu wao wa kuzungumza ukweli kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mchengerwa alionya dhidi ya kuwaruhusu Watanzania kuzoea kulishwa taarifa potofu na watu wenye nia mbaya hivyo aliwataka Maafisa Habari kwenda kutoa habari sahihi na kueleza mazuri yanayofanywa na Serikali.
“Tusiwafanye watanzania kuzoea kulishwa taarifa potofu, nendeni mkatoe ufafanuzi na habari sahihi ikiwemo kuzungumzia mazuri yanayiendelea Tanzania” alisisitiza Mchengerwa.
Mchengerwa alitaja kuwa bajeti ya TAMISEMI kwa mwaka 2025/26 ni Trilioni 11.7, ambayo ni asilimia 21 ya bajeti yote yq Serikali hivyo, alihimiza Maafisa Habari kuitangaza na kuisemea miradi hiyo kwenye vyombo vya habari .
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Mhandisi Novatus Mativila, aliwataka Maafisa Habari kufanya kazi kwa juhudi na ubunifu huku wakizingatia wakati uliopo.
Akiwasilisha mada Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba, alihimiza Maafisa Habari kuongeza ubunifu katika kazi zao, ikiwemo kutumia mitandao ya kijamii na redio.
Dkt.Rioba alisema kuwa kufanya hivyo kutasaidia kufikisha maudhui bora kwa jamii, hatua ambayo itachangia wananchi kutambua shughuli za Serikali na kuendelea kuiunga mkono.
Mwisho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.