MAANDALIZI YA NANENANE YASHIKA KASI MOROGORO.
Maandalizi ya maonesho ya wakulima ya Nanenane ya mwaka 2022 kanda ya Mashariki yameanza rasmi leo Juni 29 mwaka huu Mkoani Morogoro kwa wajumbe wake kutoka Mikoa yote minne inayounda kanda hiyo, Mikoa ya Dar es Salaam,Tanga, Pwani pamoja na Morogoro kushiriki kikao cha Kamati ya maandalizi Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akizungumza wakati wa Kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya wakulima Nanenane kilichofanyika Juni 29 mwaka huu katika ukumbi wa JKT Nanenane.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza wakati wa Kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya wakulima Nanenane kilichofanyika Juni 29 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa Kikao hicho.
Wakuu wa Wilaya za Mikoa minne wakishiriki kikao cha Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya wakulima ya Nanenane.
Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya maonesho ya wakulima kutoka Mikoa minne inayounda Kanda ya Mashariki wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho hayo kilichofanyika Juni 29 mwaka huu.
Mojawapo ya vipando vilivyopo katika viwanja vya Nanenane Mkoani Morogoro kama sehemu ya maandalizi ya Maonesho ya wakulima mwaka 2022 kwa Kanda ya Mashariki.
Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Mtunguja, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Pilli Hassan Mnyema na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albart Msando wakiwa katika kikao cha kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Wakulima.
Wajumbe wa kamati ya maandailizi wakishiriki kikao cha Maandalizi ya Maadhimisho ya Maonesho ya Wakulima nanenane yanayotarajiwa kufanyika Agosti 1 mwaka huu Mkoani Morogoro.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.