Madaktari Bingwa zaidi ya 50 waliokuwa kwenye Kambi Maalum Mkoani Morogoro kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi wamepongezwa kwa kufanya kazi kubwa na nzuri kwa siku tano tu walizofanya kazi hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa Mei10 mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima wakati wa hafla fupi ya chakula cha pomoja kilichoandaliwa naye kwa ajili ya madaktari hao wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"... Nimehemewa, nimefarijika sana kwa kazi nzuri mliyoifanya, ni jambo kubwa sana..." amesema Adam Malima.
Hata hivyo, Mhe. Malima amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaleta Madaktari hao Mkoani humo na kwamba jambo hilo ni kubwa na limeleta faraja kwa wananchi huku akitamani program hiyo kuendelea.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Pwani (Tumbi) Dkt. Aman Malima ambaye ni Mwenyekiti wa Kambi hiyo ya Kanda ya Kati, amesema lengo la awali katika program yao ni kuwaona wagonjwa 2000 hadi wanamaliza siku hizo tano wameweza kuwaona wagonjwa 3128.
Aidha, Dkt Aman aliyewawakilisha madaktari hao Bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka Pwani, Dodoma, Singida, Iringa na wenyeji Morogoro amesema lengo la awali ni kufanya upasuaji wa wagonjwa100 lakini wameweza kufanya upasuaji wa wagonjwa 109 na wagonjwa wote wametoka salama.
Pamoja na na mafanikio hayo, Dkt Amani amesema Idara ikiyoongoza ni Idara ya magonjwa yasiyoambukizwa au magonjwa ya ndani yakiwemo magonjwa ya presha hivyo akatoa wito kwa jamii kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalam wa afya kuhusu lishe au ulaji wa vyakula pamoja na kufanya mazoezi.
Kambi ya Madaktari Bingwa Kanda ya kati imefanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kuanzia Mei 6 hadi 10, 2024 ikiwa ni azma ya Serikali ya awamu ya sita inaooyongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwasogezea wananchi huduma hiyo ya Afya karibu na wananchi ili kupunguza changamoto zao za kiafya.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.