Washiriki wa mafunzo ya Mfumo mpya wa kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (National e - Procurement System of Tanzania NeST) Mkoa wa Morogoro wametakiwa kujifunza na kuelewa vema Mafunzo hayo ili kwenda kufundisha Maafisa wengine mara watakapo rejea Katika Halmashauri zao hususan Wakuu wa Idara kwa lengo la kuanza kukutumia Mfumo huo ifikapo Oktoba mwaka huu
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali watu Bw. Herman Tesha akizungumza na washiriki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo mpya wa Ununuzi wa Umma (NeST).
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali watu Herman Tesha Leo Agosti 28, 2023 alipokuwa anafungua mafunzo ya NeST yaliyofanyika Katika Ukumbi wa mikutano wa Mbaraka Mwishehe uliopo katika Manispaa ya Morogoro.
Pichani ni baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Mfumo mpya wa Ununuzi wa Umma (NeST) wakimsikiliza mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Steven Benedict.
Mafunzo hayo ni mwendelezo wa kuwajengea uwezo wataalam wa Idara mbalimbali ngazi ya Halmashauri hapa nchini juu ya matumizi sahihi ya mfumo mpya wa manunuzi (NeST) uliozinduliwa na Serikali Julai 1 mwaka huu ambapo Mkoani Morogoro yameanza kutolewa rasmi hii Leo Agosti 28.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Tawala WA Mkoa wa Morogoro Dk. Mussa Ali Mussa Bw. Herman Tesha amewataka washiriki hao wa mafunzo kutumia kikamilifu muda huo kuelewa vyema Mafunzo hayo ili kusaidia Mkoa huo kutumia Mfumo huo kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu.
Aidha, imeagizwa kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa wale watakao fanya manunuzi ya umma nje ya Mfumo wa NeST.
Afisa Tehama kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Herman Njelekela akiwaelekeza washiriki wa mafunzo hayo jinsi ya kutumia mfumo huo.
Mwaka 2019 Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ilianzisha mfumo wa kielektroniki wa manunuzi ujulikanao kama Tanzania National e-Procurement System (TANePS) kwa lengo la kuhakikisha kuwa Taasisi za Serikali zinatumia mfumo huo katika uendeshaji wa michakato ya ununuzi wa umma.
Bw. Steven Benedict ambaye ni Mkaguzi wa Ndani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akitoa mafunzo kwa washiriki wa mafunzo ya Mfumo mpya wa Ununuzi wa Umma (NeST).
Mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo ya mfumo mpya wa Ununuzi wa Umma (NeST) Bw. Leopold Ngirwa akifananua mambo mbalimbali kuhusu mfumo huo.
Aidha, Serikali ilibaini uwepo wa changamoto mbalimbali katika mfumo wa TANePS hivyo, Mwezi Julai mwaka huu ilianzisha mfumo mpya wa manunuzi wa National e-Procurement System of Tanzania (NeST) ili kukidhi mahitaji ya Nchi katika manunuzi ya umma na kukabiliana na changamoto za mfumo wa TANePS.
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Utawala na Rasilimali watu Bw. Herman Tesha (wanne kutoka kushoto waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji na washiriki wa mafunzo hayo kutoka baadhi ya Halmashauri za Mkoa huo baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.