Makatibu wa Afya hapa nchini wametakiwa kusimamia na kuzingatia kanuni, sheria na miongozo ya kiutumishi kwa kada hiyo ili kuleta ufanisi wa uwajibikaji pamoja ili kuweza kutoa huduma zenye ubora unaostahili kwa wanajamii.
Hayo yamebainishwa Juni 15 mwaka huu kupitia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Pro. Abel Makubi iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Afya Bw. Edward Mbanga alipokuwa akifungua mkutano wa mwaka wa Makatibu hao uliofanyika katika ukumbi wa Edema Mkoani humo.
Mwakilishi wa Katibu Wizara ya Afya Bw. Edward Mbanga ambaye ni mkurugenzi wa Sera na mipango wa Wizara hiyo akizungumza na Makatibu wa Afya wakati wa kufungua Mkutano wa Mwaka wa Makatibu hao uliofanyika Juni 15 mwaka huu katika ukumbi wa Edema Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa uwepo wa makatibu wa Afya nchini una manufaa makubwa kwani umechagiza mabadiliko kote nchini hasa pale wanapoungwa mkono na Serikali hali inayopelekea kurahisisha utoaji wa huduma husika kwa wananchi.
“Makatibu mnatakiwa kuhakikisha mnasimamia kwa umakini sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya kiutumishi inafuatwa na watumishi wote wa kada ya Afya ili kuleta ufanisi wa kazi” ameabinisha Bw. Mbanga.
Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa nidhamu ya kazi na uongozi jumuishi ni chachu katika kuinua ubora wa huduma za Afya hapa nchini kwani unaonesha uwajibikaji wa kufanya kazi kwa pamoja kitaasisi kwa lengo la kuongeza tija kwa jamii.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Makatibu wa ulifanyika Juni 15 mwaka huu katika ukumbi wa Edema uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Sambamba na hayo Mkurugenzi huyo amewataka Makatibu hao wa Afya kutokuwa na kigugumizi cha kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wanaonekana kwenda kinyume na maadili ya kazi kwa kuzingatia sheria zilizopo kwani kumekuwepo na malalamiko pamoja na manung’uniko juu ya uongozi shirikishi kwa watendaji.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu wa Afya Tanzania Bi. Juliana Mawalla pamoja kubainisha mafanikio ya Chama hicho, ametaja changamoto za Chama hicho ikiwa ni pamoja na baadhi ya taasisi kama vile MSD, NIMR, TMDA n.k kukosa kibali cha kuajili makatibu wa afya kutokana na Ikama zao pamoja na uwepo wa mapungufu katika taratibu za uteuzi wa wakuu wa idara ya Afya.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu wa Afya Tanzania (AHSTA) BI. Juliana Mawalla akisoma risala ya Chama hicho mbele ya mgeni rasmi wakati wa mkutano wa Makatibu hao Juni 15 mwaka huu.
Aidha Bi. Juliana ametoa mapendekezo kadhaa likiwemo la uteuzi wa wakuu wa idara za Afya yaani (DMOs na RMOs) kuweza kuzingatia vigezo vilivyowekwa ikwemo kigezo cha taaluma na uzoefu kazini.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya Bw. Edward Mbanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchama wa chama cha Makatibu wa Afya Tanzania (AHSTA).
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.