Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adamu Kighoma Malima amesema endapo Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi watakubaliana kusimamia makusanyo ya mapato ya ndani, Halmashauri hiyo ina uwezo wa kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni Nne ndani ya mwaka mmoja badala ya kukusanya shilingi bilioni 2.5 kwa mwaka.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Malinyi Mhe. Pius Mwelase wakati wa kikao.
Mhe Adam Malima amebainisha hayo Juni 6 mwaka huu wakati wa kufungua Mkutano Maaluma wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwa ajili ya kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa Serikali - CAG.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema Wilaya ya Malinyi ni moja ya Wilaya zilizojaaliwa ardhi nzuri na yenye rutuba ambayo kwayo inaweza kustawisha kila aina ya zao na kwamba malinyi inaweza kulisha mchele Tanzania nzima.
amesema kama Halmashauri ya Malinyi wataamua kwa dhati kukusanya mapato ya ndani, wana uwezo wa kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni 4 kwa mwaka, kinachohitajika ni usimamizi.
"Kama Halmashauri hii tutakaa na tukakubaliana kufanya kazi ya usimamizi, Malinyi tutatoboa bilioni 4 ndani ya mwaka mmoja na nusu au miwili" amesema Mhe. Adam Malima.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro Ndg. Solomon Kasaba akitoa salam za chama hicho wakati wa mkutano wa madiwani.
Aidha, amewataka Madiwani wa Halmashauri hiyo kusimama kidete katika kuwekeza kwenye kilimo cha mazao ya kimkakati yakiwemo zao la michikichi na karafuu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Malinyi Mhe. Pius Mwelase akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani Wilayani humo.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kushughulikia vema hoja za CAG na kuwataka kukamilisha hoja zilizosalia ili kuiweka halmashauri hiyo katika nafasi nzuri zaidi.
Hawa ni baadhi ya Waheshimiwa Madiwani katika Halmashauri ya Malinyi waliohudhuria mkutano huo.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.