• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

MASHINDANO YA MICHEZO YA MAJESHI YAPAMBA MOTO MOROGORO, MPIRA WA KIKAPU WAONESHA USHINDANI

Posted on: September 8th, 2024

Mashindano ya michezo ya majeshi hapa nchini yameendelelea kupamba moto Mkoani Morogoro ikiwa leo ni siku ya tatu tangu mashindano hayo yazinduliwe rasmi Septemba 6, 2024 huku leo mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanaume umeendelea kutisha na kuonekana ni wa kiushindani kwa timu tatu.

Mashindano hayo yamefanyika leo Septemba 8, mwaka huu  katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mkoani humo kwa kuzikutanisha timu sita zikiwemo SMZ, Magereza na  JKT.

Mashindano ya leo kwa jumla yamejumuisha timu 6 za Uhamiaji, Polisi, SMZ, Magereza, Ngome na JKT ambapo timu tatu zimetoka na ushindi ambazo ni Polisi - 63 dhidi ya uhamiaji – 52, Magereza - 78 dhidi ya SMZ - 44 na JKT - 58 dhidi ya Ngome – 57 na kuondoka na alama tatu muhimu.

Mwalimu wa mpira wa kikapu kanda wa magereza Bw. Joseph Matley amesema malengo makubwa ya timu  yao ni kupata matokeo hususan wachezaji kucheza kwa kufuata maelekezo na kujituma wakiwa uwanjani hivyo imefanya mchezo kuonekana mzuri na wa kufurahisha.

Kwa upande wake, Mwalimu wa Timu ya mpira wa kikapu wa SMZ Bw. Seif Issa Omary amesema kuwa hawajafanya vizuri kwa sababu ya kuzidiwa kimbinu na kupoteza mchezo huo huku akisema tayari wachezaji wamejipanga kufanya vizuri mchezo ujao.

Naye, Nahodha wa Timu ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Bw. Felix Deogratius amesema mchezo huo ulikuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana na kuwa na waalimu wazoefu wa pande zote pamoja na uwezo wa wachezaji mahiri lakini mchezo umeamua kwa timu hizo tatu kuondoka na ushindi.

 MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.