MBIO ZA MWENGE WA UHURU KUMULIKA MIRADI YA MAENDELEO 68 MKOANI MOROGORO.
Mwenge wa Uhuru 2023 unatarajiwa kuanza kukimbizwa Mkoani Morogoro kuanzia Mei 6 hadi 14 mwaka huu ambapo unatarajiwa kupitia miradi ya maendeleo 68 yenye thamani ya zaidi ya Tsh Bil. 12.1.
Miongoni mwa miradi ambayo itapitiwa na Mwenge wa Uhuru kutoka sekta mbalimbali ikiwemo elimu, maji, Afya na barabara.
MWENGE wa Uhuru ambao unatoka kukimbizwa Mkoani Iringa utapokelewa Mkoani humo katika Kata ya Chita na kukimbizwa katika Halmashauri zote 9 za Mkoa wa Morogoro na utakabidhiwa Mkoa wa Pwani hapo Mei 15 mwaka huu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Bw. Abdallah Shaib Kaim (katikati).
Taarifa iliyotolewa inaeleza kuwa Mwenge wa Uhuru utapitia jumla ya miradi 68 yenye thamani ya Shilingi 12,170,922,197.46 kwa ajili ya Ufunguzi, Uzinduzi, uwekaji mawe ya msingi na kukagua.
Aidha, miradi 24 itawekewa jiwe la msingi, 5 itafunguliwa, 19 itazinduliwa na miradi 20 itakaguliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa ataongoza mapokezi ya Mwenge huo wa Uhuru katika kata ya Chita ukitokea Mkoani Iringa.
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 zinaenda sambamba na kaulimbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.
Hima hima wanamorogoro tushikamane kuupokea mwenge wa Uhuru popote utakapopita.
Morogoro nguvu moja ushindi Kwetu ni Tania yetu
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.