Mbui wa jadi aguswa na uongozi wa Mama Samia, amshukuru, amwombea
Mbui wa Jadi wa kabila la wapogolo Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake Madhubuti wa kuwasogezea wananchi huduma za kijamii karibu yao.
Mbui huyo wa jadi aliyejitambulisha kwa jina la Paulo nziman mkazi wa Kijiji cha Ruaha ametoa pongezi hizo Juni 6 mwaka huu alipofika eneo la ujenzi wa kituo cha Afya cha Ruaha siku ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima kukagua utekelezaji wa mradi huo.
Mbui huyo mara alipokutana na Mkuu wa Mkoa alimpa Mkuu wa Mkoa mbuzi kama alama ya shukrani kwa uongozi mahili wa Dkt. Samia Suluhu Hassan huku akisisitiza kuwa uongozi wa kiongozi huyo hauna shida.
"nashukuru uongozi wake mzuri hauna shida, namwombea na mimi naomba aniombee" alibainisha Kiongozi huyo wa jadi.
Mbui huyo alifika eneo la ujenzi kuunga mkono juhudi za Mhe. Samia Suluhu Hassan za kuwaletea wananchi wa eneo hilo maendeleo kwa kuwajengea kituo cha Afya.
Aidha, alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa amemuunga mkono mama kwa kuchangia saruji mifuko nane jambo ambalo lilimsisimua Mkuu wa Mkoa Adam Malima na yeye kumuunga mkono Mbui huyo kwa kutoa mifuko ishirini ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo hicho.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.