Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga amezipongeza Halmashauri za Mkoa wa Morogoro kwa kushiriki kikamilifu kwenye mashindano ya Michezo ya shule za Msingi UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa yaliyofanyika katika Halmashauri hiyo tangu Mei 30 mwaka huu.
Mhe Kihanga amesema hayo hii leo wakati anafunga rasmi mashindano hayo katika uwanja wa Jamhuri uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kwa michezo hiyo inaongeza urafiki baina ya washiriki wa michezo hiyo.
Mhe. Kihanga amesema mashindano yanaleta umoja na ushirikiano kwa sababu watu mbalimbali kutoka Halmashauri zote za Mkoa hu zinakusanyika pamojana kutumia fursa kujuana na kuweza kuongeza marafiki
Katika hatua nyingine, Mhe. Pascal Kihanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro - MRFA amewapongeza waandaji wa mashindano hayo kwa kwa ngazi zote kwa kuyaratibu vizuri na umakini mkubwa.
Kwa upande wake Bi. Arisi Mushi mwalimu wa shule ya msingi ya Mgolole iliyopo Manispaa ya Morogoro akiongea kwa niaba ya walimu waliosimamia mashindano hayo amesema licha ya kuwa na changamoto mbalimbali, uongozi umeweza kuyasimamia vizuri hivyo kupelekea watoto kufurahia mashindano hayo.
Naye Mwajuma Hassan mwanafunzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Gairo akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake mesema, mashindano hayo yameongeza ujuzi wa kipaji chake cha kucheza mpira wa mikono huku akiwasihi wanafunzi wenzake wasikate tamaa hata kama hawajachaguliwa kuendelea na mashindano kwenda ngazi ya kitaifa, waendelee kufanya mazoezi kwa bidii ili nao mashindano yanayokuja waweze kuchaguliwa.
Mashindano hayo ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa yalihusisha michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu, riadha, volleyball wasichana na wavulana, kwaya, ngoma, mziki wa kizazi kipya na mpira wa kikapu kwa wasichana na kwa wavulana.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.