Mfumo mpya wa PEPMIS kuongeza uwajibikaji Serikalini.
Kuanzishwa kwa mfumo mpya wa Public Employee Performance Management Information System – PEPMIS una lengo kuongeza ufanisi na uwajibikaji kwa watumishi wa Serikali hapa nchini.
Hayo yamebainishwa Januari 24, 2024 na Bw. Paul Magesa ambaye ni Mwezeshaji wa mfumo wa PEPMIS kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi kwenye kikao cha majumuisho ya mafunzo ya utekelezaji wa mfumo huo wa PEPMIS.
Bw. Magesa amesema kuwa mfumo huo umeanzishwa kwa lengo la kupima na kutathmini utendaji kazi wa Watumishi wa Serikali katika Taasisi mbalimbali za Umma, hivyo mfumo huo unatarajia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa watumishi hao.
“...mfumo huu tunatarajia kuwezesha watumishi kuwajibika kwa hiyari na hatimae kuleta ufanisi na tija Serikalini...” amesema Bw. Magesa.
Aidha, ameeleza kuwa kwa Mkoa wa Morogoro Zaidi ya asilimia 80 ya Watumishi wa Umma kutoka taasisi 25 wamesajiliwa katika mfumo huo huku akiamini kuwa baada ya wiki moja Mkoa huo utafikia aislimia 100 ya watumishi waliosajiliwa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Bw. Ally Machela kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kikao hicho amewashukuru wawezeshaji wa mfumo huo na kuwasisitiza watendaji wengine kuhakikisha kuwa hadi kufika Januari 31, 2024 wanawasajili watumishi wao kwenye mfumo ili kuzifikia asilimia 100 za utekelezaji.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.