MGANGA MKUU MKOA WA MOROGORO DKT. URIO KUSIRYE AWATAKA WATENDAJI MKOANI HUMO KUJIPANGA KWA CHANJO
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Urio Kusirye amewataka watendaji na wataalamu Mkoani humo kujipanga katika utekeleza kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa polio ya matone inayotarajiwa kuanza Aprili 28 MWAKA huu kwa nchi nzima inayohusisha watoto walio chini ya miaka mitano hata kama watoto hao walishapata chanjo hiyo siku za nyuuma.
Dkt. Urio Kusirye
Akiongea na hadhira hiyo Dkt. Kusirye amesema Kampeni hiyo imekuja kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Polio uliotokea nchi jirani ya Malawi.
Mratibu wa Magonjwa ya chanjo Mkoa wa Morogoro Dkt. Masumbuko (Kushoto)
Pamoja na maagizo hayo aliyoyatoa katika kikao cha mafunzo kwa timu za Uendashaji wa huduma za Afya ngazi ya Wilaya ama Halmashauri za Wilaya kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kusirye amewataka watendaji hao kuhakikisha wanashika kile wanachofundishwa lakini chonjo hiyo inakuwa endelevu.
mmoja wa watoa mada katika kikao hicho
baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Kampeni ya chanjo ya Polio ya matone
baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Kampeni ya chanjo ya Polio ya matone
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.