Miradi ya Tsh Bil. 19.9 itapitiwa na Mwenge Mkoani Morogoro
Mwenge wa Uhuru mwaka, 2024 utapokelewa Mkoani Morogoro Aprili 20, 2024 na utakimbizwa umbali wa Km 1,730. Kwq Mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini Kwake, Mwenge huo utapitia jumla ya Miradi 70 yenye thamani ya Tsh Bil. 19.9 ambapo miradi 18 itawekewa mawe ya msingi, 11 itafunguliwa,18 itazinduliwa na miradi 23 itakaguliwa na kuonwa.
Mwenge huo utapokelewa Aprili 20, 2024 katika Wilaya ya Mvomero ukitokea Mkoa wa Tanga na utakimbizwa Wilaya zote saba (7) za Mkoa huo zenye Halmashauri tisa (9) na kuhitimisha mbio hizo Mkoani Morogoro, Mwenge huo utakabidhiwa Mkoani Pwani aprili 29, mwaka huu ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro DC.
Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu 2024 unatimiza miaka 60 tangu uanze kukimbizwa hapa Nchini, miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Wananchi wote wa Mkoa wa Morogoro na viunga vyake, mnaombwa kushiriki kikamilifu katika kuupokea, kuukimbiza na kukesha na Mwenge huo wa Uhuru katika maeneo yote ambapo Mwenge huo utapita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.