• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

MIZENGO PINDA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI, ASISITIZA USHIRIKIANO

Posted on: August 2nd, 2025



Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, amefungua rasmi maonesho ya  Nanenane Kanda ya Mashariki huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na kupeana uzoefu na mawazo yatakayoleta mabadiliko katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.

Mhe. Pinda amesema hayo Agosti 2, 2025, wakati akifungua maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere mkoani Morogoro, ambapo kaulimbiu ya maonesho hayo inasema, “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, 2025”.

Mhe. Mizengo Pinda amesema kuna umuhimu wa sekta binafsi na umma kuwa na ushirikiano wa karibu na kufanya kazi pamoja hususan katika nyanja za ufugaji, kilimo na uvuvi ili kuweza kuongeza thamani ya mnyororo wa mazao yatokanayo na sekta hizo kwa maslahi mapana ya taifa.

“Niwaombe sana wananchi: ushirikiano, ushirikiano miongoni mwetu; jambo la msingi sana,” amesema Mhe. Mizengo Pinda.

Aidha, Mhe. Pinda amesema ili kuwaletea maendeleo watanzania, lazima kuishirikisha Sekta binafsi kwa kuwapatia maeneo ya uwekezaji, Pia amewataka wananchi kuachana na jembe la mkono badala yake watumie zana bora za kilimo, mifugo na uvuvi zinazooendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Sambamba na hayo, Mhe. Mizengo Pinda amebainisha mazao yaliyoongoza kuingiza fedha kupitia mauzo ya nje hivyo kuchangia pato la Serikali kwa kipindi cha mwaka 2022 hadi 2025 kuwa ni pamoja na zao la ufuta limeingiza zaidi ya sh. trilioni 2.2, korosho sh.Bi. 931, tumbaku zaidi ya sh. Bil. 800, na mengine yaliyoongezwa thamani kupitia mfumo wa stakabali za ghala.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu huyo Mstaafu amewakumbusha wananchi kujitokeza na kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, kwani ni haki yao ya Msingi kumchagua viongozi wao ili waweze kuwaletea maendeleo katika maeneo yao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, amemshukuru Mhe. Pinda kwa kukubali kushiriki ufunguzi wa maadhimisho hayo, pia amesema wataendelea kujipanga kuhakikisha maonesho yajayo yanakuwa mazuri kuliko yaliyopita.

Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki kwa mwaka huu wameandaa jukwaa la mafunzo ya mbinu bora za kilimo, mifugo na uvuvi, hivyo wananchi na wadau mbalimbali wameaswa kufika na kupata elimu ya sekta hizo ili ziweze kuleta tija zaidi.


Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • Mhe. Rais afanyiwa tambiko na wazee wa kimila Morogoro

    August 28, 2025
  • RC Malima atoa siku saba kuunda SACCOS

    August 22, 2025
  • SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA VIJANA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO

    August 12, 2025
  • WADAU WA MAONESHO YA NANENANE WAAGIZWA KUTEKELEZA WALIYOJIFUNZA

    July 12, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.