Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda amefurahishwa na ujenzi wa kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kinachomilikiwa na serikali kwa 100%, huku idadi kubwa ya wafanyakazi wake wakiwa ni wazawa.
Mhe. Mizengo Pinda amesema hayo Leo Agosti 2, 2023 alipotembelea Kiwanda cha sukari cha Mkulazi kilichopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kwa lengo la kujionea ujenzi wa Kiwanda hicho huku akionesha kuridhihwa na hatua iliyofikiwa.
Mhe. Mizengo Pinda pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika kiwanda kipya cha sukari cha Mkulazi kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho.
Aidha, Mhe. Pinda amesema uchumi wa wananchi utaongezeka sana kwa sababu serikali imeanza kuwekeza na kuwashirikisha vijana na wanawake kwenye kilimo hususani kilimo cha miwa ili kuweza kulisha viwanda vya sukari na kupata sukari ya kutosha.
Katika hatua nyingine Mhe. Pinda amepongeza juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nia yake ya kutokuagiza sukari nchi za nje.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kutembelea Taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) Wilayani Kilosa.
Kwani amesema ni jambo la kujivunia kwa Serikali kuwa na uwekezaji mkubwa wa viwanda vya Sukari hapa nchini.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema ukamilishaji wa kiwanda hicho utasaidia nchi katika mahitaji ya sukari tani 550,000 hadi 600,000 kwani Morogoro pekee itakuwa inatoa tani 430,000 ndani ya mfumo, hivyo amepongeza uongozi wa kiwanda hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akimuonesha Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda vitalu vya miche ya michikichi ambayo itagawanywa kwa baadhi ya Halmashauri kwa ajili ya kupandwa.
Hata hivyo, Mhe. Malima amefurahishwa na mpango mkakati wa kiwanda hicho kushirikiana na wakulima wa miwa ili kuzalisha malighafi za kutosha za kulisha kiwanda sambamba na kupata ujira wao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.