MJADALA WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA WAHITIMISHWA, MOROGORO YAAZIMIA..
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Abubakar Mwassa akifuatilia mjadala wa Nishati safi ya kupikia kwa njia ya mtandao (mubashara) kutoka Dar es Salaam
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa akiweka kumbukumbu sahihi yale machache aliyopata kwenye mjadala huo
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Mathayo Massele akihitimisha mjadala wa nishati safi ya kupikia Mkoani Morogoro kwa niaba ya Mkuu wa MKoa huo
Baadhi ya Wahe. Wakuu wa Wilaya wakifuatilia kwa makini Mjadala wa Nishati Safi ya kupikia
wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri wakifuatilia mjadala huo
Baadhi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa wakishiriki pia mjadala wa nishati safi ya kupikia
Makatibu Tawala wa Wilaya ya Malinyi na Ulanga wakifuatilia mjadala kwa umakini mkubwa, ni ukweli usiopingika mjadala huu umewagusa watu wengi
Mjadala wa siku mbili uliohusu Nishati safi ya kupikia ambao umeandaliwa na Wizara ya Nishati, kufanyika Jijini Dar es Salaam na Mikoa mingine ya Tabora, Dodoma, Iringa, Shinyanga na Morogoro kushiriki kwa njia ya mtandao umetamatika Novemba 2 mwaka huu.
Mkoa wa Morogoro wenyewe umeazimia suala hilo la Nishati safi ya kupikia iwe ni ajenda ya kudumu, kuendelea kuzungumzwa kwenye vikao vyote vya kisheria kwa lengo la kutafuta mbinu mbadala lakini pia kutoa uelewa kwa wananchi wake kuhusu madhara ya matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia.
Kauli ya azimio hilo imetolewa na Mhe. Mathayo Maselle Mkuu wa Wilaya ya Malinyi kwa niaba ya Mkuu wa MKoa huo Mhe. Fatma Abubakar Mwassa alipokuwa anafunga mjadala huo hapa Mkoani Morogoro na kuwashukuru wadau mbalimbali kwa kushiriki mjadala huo muhim uliofanyika katika hoteli ya Morena Mjini Morogoro.
“...Jambo hili tunaposubiri maelekezo muhim, basi tuifanye kama ajenda ya kudumu, kila mahali tunapokwenda kwenye mikutano yetu katika ngazi ya Wilaya ngazi ya Kata na ngazi za Vijiji iwe ajenda ya kudumu tuizungumze...” ameagiza Mhe. Mathayo Maselle.
Jijini Dare es Salaam, akihitimisha mjadala huo Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba amesisitiza namna atakavyotekeleza Maagizo ya Mhe, Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa Novemba 1 mwaka huu wakati akifungua mjadala huo.
Baadhi ya maagizo hayo ni pamoja na kuunda kikundi kazi kitakachohusika au shughulikia Nishati Safi ya Kupikia, kuanzisha mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia na kuondoa wavamizi wote wa vyanzo vya maji hususan katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Bw. Aristotle James Afisa Masoko wa kampuni ya Viridium Tanzania Limited akitoa maelezo kwa washiriki namna ya kutumia majiko na nishati ya mkaa mweupe ambao unazalishwa na Kampuni hiyo.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Miundombinu Mkoa wa Morogoro Mhandisi Ezron Kilamhama (kulia) akipokea jiko la kupikia na mkaa mweupe kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi ambavyo ni salama na havina madhara kwa mazingira na binadamu
Afisa Wanyama Pori Mkoa wa Morogoro Joseph Chuwa (kulia) akipokea jiko la kupikia linalotumia mkaa mweupe, tayari kwa matumizi ya nishati safi ya kupikia
baadhi ya washiriki kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali na za binafsi walishiriki kikamilifu mjadala huo hapa Morogoro
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.