Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kuibuka mapigano kati ya wafugaji jamii ya kimasai kutaka kuiba mifugo ya wafugaji jamii ya wasukuma katika mashamba ya wakulima kijiji cha tindiga tarafa ya Masanze Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.
Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela leo Julai 25, 2021 ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani humo kuwatafuta watu wote walioshiriki katika vurugu hizo na kusababisha kifo cha John Nyerere ambaye ni mfugaji wa jamii ya kisukuma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.