• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Morogoro kuwa kitovu cha uzalishaji wa mazao ya viungo

Posted on: January 26th, 2024

Morogoro kuwa kitovu cha uzalishaji wa mazao ya viungo.

Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa amesema mkoa wa Morogoro umejipanga kwa ajili ya kilimo cha mazao ya viungo hususan Karafuu ili kuongeza kipato cha Wananchi wa Mkoa huo na taifa kwa jumla lakini pia lengo likiwa ni kurudisha uoto wa asili katika milima ya Urugulu.

Dkt. Mussa Ali Mussa ametoa kauli hiyo Januari 25, 2024 wakati wa kikao cha Wizara ya Kilimo cha kutambulisha mradi wa uzalishaji wa miche ya mikarafuu kilichofanyika  katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kikao kilichoratibiwa kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo.

Amesema, kwa kushirikiana na mashirika mengine yakiwemo Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA) watatoa bure kwa wananchi miche ya mazao ya Viungo ikiwemo miche ya mikarafuu ili waweze kupanda katika milima ya Uluguru zao litakalokuwa rafiki kwao hivyo kusaidia kutunza mazingira ya milima hiyo.

"milima ya Uluguru inakabiliwa na uharibifu wa mazingira kwa kukata miti ovyo, kwa kupanda mazao hayo ya Karafuu itapelekea wananchi kutokata miti hiyo kwa kuwa inawaingizia kipato na wakati huo itahifadhi mazingira". Amesema Dkt. Mussa.

Katika Hatua nyingine Dkt. Mussa amesema kuwa,  Mkoa huo umeanza kujenga maghala ya kuhifadhia karafuu ili kuwa na sehemu moja ya kuuzia zao hilo, na kusaidia Halmashauri ya Wilaya  ya Morogoro kuweza kusimamia na  kukusanya mapato yake vizuri.

Aidha, amesema, Wananchi wameweza kuhamasika na kuanza kupanda miche ya mikarafuu pamoja na kuzalisha miche hiyo si chini ya laki 4, hivyo kama mkoa wanajipanga ili kwenda kununua miche hiyo iliyozalishwa na wananchi na kuigawa kwao ili waipande.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Uzalishaji wa Mazao  Wizara ya Kilimo Bi. Beatrice Banzi amesema lengo la kikao hicho inatokana na utafiti uliofanywa na Wizara hiyo siku za nyuma baada ya  Mkoa wa Morogoro kuonesha nia ya kulima zao hilo.

Kwa sababu hiyo wizara ilifanya utafiti na kugundua kuwa sehemu kubwa ya Mkoa huo inaweza kustawisha zao la karafuu hivyo kuongeza kipato cha wananchi na kuhifadhi mazingira kwa sababu miti ya mikarafuu hafyuzi maji.

Katika utekelezaji wa azma hiyo, Wizara imetafuta miche 235,000 ya mikarafuu kwa ajili ya kupandwa mkoani humo. Bi. Beatrice amebainisha kuwa kabla ya kupewa miche hiyo baadhi ya wakulima watapelekwa kupata mafunzo ya siku tatu katika kituo cha kuzalisha miche cha Mlingano cha Mkoani Tanga ili kupewa ujuzi wa kustawisha zao hilo na baada ya mafunzo hayo watapewa miche hiyo tayari kwa kupandwa.  

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji  Mali Dkt. Rozalia Rwegasira amesema yeye pamoja na watendaji wenzake wa Sekta ya Kilimo na Uchumi watahakikisha wanatekeleza maono ya Mkoa huo kustawisha mazao ya viungo ikiwemo zao la karafuu hivyo kujulikana kama Morogoro Spice Aroma  Hub lakini pia kurudisha uoto wa asili wa Mlima ya Uluguru.

Naye Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Chesko Lwaduka amesema katika kuongeza thamani ya mazao ya viungo yakiwemo iliki, mdalasini tangawizi,vanila karafuu na Pilipili manga kwa mwaka 2023 wameweza kusambaza bure kwa wananchi miche 30,000 ya mikarafuu pamoja na kuandaa kitalu kingine cha miche 100,000 kwa ajili ya mwaka ujao.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.