Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela amewataka viongozi wa Mkoa huo kuweka mipango mikakati itakayo wezesha Mkoa huo kuwa Jiji kutokana na rasilimali mbalimbali zinazopatikana Mkoani humo.
Mhe. Shegela ametoa agizo hilo Mei 20 mwaka huu wakati wa makabidhiano ya Ofisi kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Loata Ole Sanare yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
‘’….Tuweke mikakati ya kuitoa Morogoro hapa ilipo, na moja ya mkakati ni kuufanya Mkoa huu kuwa Jiji, tukiweka malengo hakuna sababu zozote za kutoufanya Mkoa huu kuwa Jiji…..’’ Amesema Mhe. Shigela.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.