• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

MOROGORO YAPANIA KUKUZA SEKTA YA BIASHARA, KUVUTIA WAWEKEZAJI.

Posted on: June 16th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adama Malima amesema sekta ya biashara ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi hapa nchini hivyo amewataka wadau wa uchumi kushikamana katika kuweka mazingira ambayo yanavutia wawekezaji ili kuinua uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akizungumza na wadau wa sekta ya biashara wakati akifungua mkutano wa Baraza la biashara la Mkoa wa Morogoro.

Mhe. Adam Malima ametoa kauli hiyo Juni 15 mwaka huu kwenye mkutano wa Baraza la Biashara la Mkoa uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Morena uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema uwepo wa mazingira mazuri ya biashara huvutia wawekezaji na kufanya ukuaji wa pato la Mkoa kutokana na ushuru na kodi mbalimbali zinazokusanywa kutoka kwa wafanya biashara.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (kulia) akiwa na Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Utawala na Rasilimali watu Bw. Herman Tesha wakati wa mkutano wa baraza la biashara.

“...tuendane na malengo yetu ya kutengeneza mazingira wezeshi, mazuri zaidi ambayo ndiyo msingi wa maelekezo ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan...” amesema Mhe. Adam Malima.

Aidha, amewataka wakuu wa taasisi za umma na binafsi kufanya kazi kwa umoja kwa kuthamini mchango unaotolewa na kila mmoja ili kufanikisha maendeleo ya Mkoa huo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amemshukuru na Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya kuondoa changamoto za uwekezaji na kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi.

Naye Mkurugenzi wa idara ya masoko kutoka Kampuni ya Sukari Kilombero Bw. Fimbo Butallah amesema wataendelea kudhamini mikutano ya biashara ili kufungua fursa za kiuchumi za Mkoa huo.

Huyu ni Mkurugenzi wa idara ya masoko kutoka Kampuni ya Sukari Kilombero Bw. Fimbo Butallah.

Aidha, ameongeza kuwa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kinafanya upanuzi wa kiwanda ili kuongeza uzalishaji wa sukari na kutoa fursa za ajira kwa wananchi wa Mkoa huo. sambamba na kutoa ajira kiwanda kinapata malighafi ya miwa kutoka kwa wakulima 8,000 ambao wanazalisha tani 600,000 za miwa kwa mwaka.

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Viwanda, Biashara na uwekezaji Bi. Beatrice Njawa (wa kwanza) akiwa kwenye mkutano wa baraza la biashara.

ameongeza kuwa, kupitia upanuzi wa kiwanda hicho watahitaji nyongeza ya wakulima 1,400 ili kufikisha tani 1,500,000 za miwa kwa mwaka na kukidhi mahitaji ya kiwanda hicho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga Bw. Faustini Almas amezilalamikia Halmashauri za Mkoa huo kwa kile alichodai kutoshirikishwa kwenye masuala yanayowahusu maendeleo ya  Mkoa huo.

Baadhi ya wajumbe wa baraza la biashara wakichangia hoja wakati wa mkutano huo wa baraza la biashara.


MWISHO.



Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.