• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Mradi wa TMCHIP kwenda kuboresha afya ya mama na mtoto

Posted on: December 12th, 2024

Mradi wa mpango wa uwekezaji wa huduma ya Mama na mtoto (TMCHIP) umelenga kuboresha afya ya Mama na mtoto pamoja na wananchi wote kwa kuboresha miundombinu yakiwemo majengo, ajira, uboreshaji wa huduma za rufaa na kununua vifaa na vifaa tiba ili kuwa na huduma za uhakika hususan za kundi hilo hapa nchini.

Hayo yamebainishwa Disemba 12, Mwaka huu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi, ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe wakati akifungua mafunzo ya utekelezaji wa mradi wa TMCHIP katika ukumbi wa hoteli ya Cherry iliopo Mkoani Morogoro yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo na kuongeza uelewa wa watendaji na wataalam wa sekta ya afya.

Akifafanua zaidi Naibu katibu huyo, amesema mradi huo unaogharimu zaidi ya Tsh. Bil 16 unalenga kupunguza vifo vya Mama na mtoto ambapo hadi sasa imepunguza kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mpaka 104 kwa kila vizazi hai 100,000 ikiwa ni zaidi ya 80%, hivyo mradi huo una malengo mahsusi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

"...Mradi huu ambao tunaongelea hapa ni mradi ambao umejikita kuboresha afya ya Mama na mtoto lakini sio afya ya Mama na mtoto pekee bali na afya ya wanannchi wote..." amesema Dkt. Grace Magembe

Aidha, Dkt. Grace amesema mradi huo umepanga kutoa ajira kwa watumishi 1000 ambapo mpaka sasa mradi huo wameajiriwa watumishi 700 na ajira 300 kutangazwa hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, Dkt. Magembe amewataka wataalam na wasimamizi hao kusimamia vema miundombinu inayojengwa na mradi huo kwa kutekeleza kwa ufanisi na kuzingatia thamani ya fedha kuendana na ubora wa mradi (Value for money) ili kuwa na miundombinu bora itakayotumika kizazi cha sasa na kijacho.

Sambamba na hayo Dkt. Magembe amewasisitiza kuwa, katika kutekeleza miradi hiyo waepuke uharibifu wa mazingira ili kumuunga Mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupiga vita uharibifu wa mazingira huku akiwataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha maeneo yanayopendekezwa kutekeleza miradi husika yawena hati ili kuepuka migogoro baada ya mradi kuanza kutekelezwa.

Kwa upande wake, Mratibu wa mradi wa TMCHIP Dkt. Athuman Pembe amesema mradi huo wa miaka mitano ulioanza mwaka 2023 utatekelezwa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na kubainisha kuwa mradi huo utatekelezwa katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Halmashauri zaidi ya 101.

Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Best Richard Magoma ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuboresha mazingira ya sekta ya afya ambapo huduma ya miaka sita iliyopita inatofautiana sana na ya sasa kwa kuwa miundombinu ya sasa imeboreshwa na kuwafanya wananchi kutotembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo kwa kuwa hata huduma za rufaa zinapatikana kwenye Hospitali za Wilaya.

Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.