• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Msaada wa kisheria

Posted on: September 29th, 2021

Utoaji wa Msaada wa Kisheria utapunguza msongamano magerezani

Jeshi la Magereza hapa nchini limetakiwa kushirikiana na wadau wanaotoa msaada wa kisheria ikiwemo Asasi ya kiraia ya EnviroCare ili kulifanya jeshi hilo kupunguza msongamano wa wahalifu walioko kwenye vizuizi wakiwemo mahabusu na hivyo kuimarisha uchumi wa jeshi hilo na Taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela Septemba 29 mwaka huu Wakati akifungua semina ya mafunzo ya utoaji wa huduma za msaada wa kisheria katika maeneo ya vizuizi wakiwemo mahabusu yanayofanyika kwa siku tatu katika Hoteli ya Kings way katika Halmashauri ya manispaa ya Morogoro.

Martine Shigela pamoja na kulipongeza jeshi hilo kwa kufanya kazi kwa karibu na InviroCare na amelitaka kuendeleza ushirikaiano huo ili mahabusu na wafungwa waweze kupata msaada wa kisheria hivyo kupunguza msongamano uliopo katika magereza kwani wengi wao wanaweza kupata dhamana kwa makosa yao na kupunguza misongamano hiyo.

Akifafanua zaidi Martine Shigela amesema takwimu zinaonesha kuwa ndani ya magereza hapa nchini mahabusu ni wengi kuliko wafungwa na kwa mujibu wa Sheria za Tanzania Mahabusu hawaruhusiwi kufanya kazi za uzalishaji isipokuwa mfungwa, hivyo, wafungwa wamekuwa wakifanya kazi ya ziada katika kuzalisha kwa ajili yao na kwa ajili ya mahabusu jambo linalorudisha nyuma kiuchumi Jeshi hilo.

 “…Ni kwamba tuna mahabusu wengi ambao hawazalishi ukilinganisha kati ya wafungwa wanaofanya kazi na mahabusu pamoja na walioko kwenye vizuizi 40% ni wafungwa wakati 60% ni mahabusu… kundi hili kwa mujibu wa Sheria zetu hawatakiwi kufanya kazi” amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Naye Msajiri wa watoa huduma za Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Felista Mushi amesema kwa sasa msaada wa kisheria umevuka kutoka kuwa huduma kwa watu walioko vizuizini kuwa ni haki kwao kama zilivyo haki nyingine bila kujali mhusika amefanya makosa na yuko kizuizini.

Amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado inamruhusu mtu huyo kupata haki yake ya Msaada wa kisheria ikiwemo kukata rufaa au kudhaminiwa na kwa kupitia msaada huo mtuhumiwa anaweza kufikia malengo anayoyatarajia ya kupata haki yake.

Katika hatua nyingine Bi. Felista ametumia fursa hiyo kwa niaba ya Wizara ya Katiba na Sheria kulipongeza Jeshi la Magereza hapa nchini kwa kuonesha ushirikiano mkubwa katika kuwafikishia Msaada wa Kisheria watu walioko katika vizuizi hususan wakati wa maadhimisho ya msaada wa kisheria  wakiwemo mahabusu na wafungwa magerezani na hivyo husaidia kupunguza msongamano magerezani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa InviroCare ambao ndio  walioandaa mafunzo hayo Bi. Catherine Jarome ametaja mafanikio ya Asasi hiyo kuwa ni pamoja na kuazisha mitandao ya wasaidizi wa kisheria kikanda, kutoa mafunzo kwa wasaidizi wa Kisheria 272 wakiwemo Askari Polisi, Askari magereza na Mahakimu 40 huku msaada wa kisheria ukiwa umetolewa kwa mahabusu zaidi ya elfu thelathini.

Akitoa shukrani mara baada ya Hotuba ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Morogoro SACT Rajab Hamza, amesema jeshi la Magereza wanakubaliana kabisa na wito uliotolewa na Mkuu wa Mkoa kuwa moja ya njia ya kupunguza Msongamano wa mahabusu utoaji wa huduma ya Msaada wa kisheria.

Aidha, amesema Jeshi hilo halifurahishwi kuwa na mahabusu wengi ambao kimsingi wanazuiliwa kisheria kufanya kazi zozote za uzalishaji hivyo wangefurahishwa kuona watuhumiwa hao ama wanaachiwa kuwa huru kwa mujibu wa taratibu ili kwenda kuzalisha wakiwa uraiani ama wanatiwa hatiani kwa mujibu na kufungwa ili waingizwe kwenye utaratibu wa uzalishaji na hatimae jeshi hilo kujitegemea.

Mradi huu wa kutoa Msaada wa Kisheria ulianza mwaka 2012 na shirika lisilo la Kiserikali la InviroCare lengo likiwa ni kutoa msaada wa kisheria kwa walio maeneo ya vizuizi, na mwaka 2017 Serikali ilitunga sheria ya msaada wa kisheria kwa lengo la kuratibu na kusimamia masuala yote yanayohusu utoaji wa msaada wa kisheria hapa nchini. Ndani ya sheria hii kuna kipengele kinachotaka maeneo yote ya vizuizi ikiwemo Polisi na magereza kutoa mazingira rafiki kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria kwa wahitaji.

Kikao hicho kinalenga kutoa mafunzo kwa Wakuu wa Magereza na wanasheria wa magaraeza hayo kwa mikoa 9 ya mradi ambayo ni Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Geita, Mawanza, Tabora, Kilimanjaro, Tanga na mwenyeji wao Mkoa wa Morogoro.

 

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.