Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amewataka Maafisa Habari wa Mikoa, Halmashauri na Taasisi zilizo chini ya TAMISEMI kufanya kazi zao kimkakati ili kutekeleza azma na maono ya Serikali ya awamu ya sita.
Msigwa ametoa rai Mei 25, 2025 wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha Maafisa habari wa tawala za mikoa, halmashauri na taasisi zilizo chini ya TAMISEMI, kilichofanyika tarehe 23.05.2025 na 24.05.2025 katika ukumbi wa Jiji la Dodoma mji wa Serikali Mtumba.
"Nakuomba tukafanye kazi zetu kimkakati ili kufikia malengo ya serikali na taasisi mnazofanyia kazi" amesema Msigwa.
Aidha, Katibu Mkuu huyo amekemea kasumba ya baadhi ya Viongozi wa Halmashauri wanaodhani vitengo vya Mawasiliano Serikalini havihitaji fedha. Amesema katika mwaka huu wa uchaguzi mkuu viongozi hao wahakikishe Maafisa habari wanawezeshwa fedha na kwenda kwenye vyombo vya habari kueleza mazuri ambayo serikali imeyatekeleza katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine, Msigwa amewajulisha maafisa habari jukumu jipya la usimamizi na uratibu wa masuala ya mitandao ya kijamii ambalo Idara ya Habari Maelezo imekabidhiwa na kuwataka maafisa husika wenye changamoto katika eneo hilo wawasiliane na habari maelezo ili kupata msaada na kuzilinda akaunti za social media za taasisi zao dhidi ya watu wenye nia ovu.
Mwisho
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.