Mtume Boniface Mwamposa amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima leo Novemba 25, 2023 na kuzungumza mambo mbalimbali ya kimaendeleo.
Pamoja na kuonekana wawili hao wamekuwa marafiki wa ukaribu kwa siku nyingi, wametumia fursa ya kukutana kwao kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya wananchi wa Mkoa wa morogoro na watanzania kwa jumla huku Mhe. Malima akimpongeza Mtume Mwamposa kwa mahubiri yake ambayo amesema yanadumisha amani, upendo na ushirikiano ndani ya jamii.
Kwa upande wake Mtume Boniface Mwamposa amempongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa kuendelea kuaminiwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kwamba hiyo ni ishara tosha kuwa Serikali yake inamwamini.
Pamoja na shukrani na pongezi hizo Mwamposa amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa ombi lake la kuongeza wigo wa huduma yake katika maeneo mengine Mkoani humo hasa maeneo ya pembezoni mwa Manispaa ya Morogoro atalifanyia kazi ili kuweza kuzifikia Wilaya zote za Mkoa huo na Tanzania nzima.
Mtume Boniface Mwamposa alikuwa Mkoani Morogoro kwa siku tatu tangu 23 hadi leo 25 kwa ajili ya kuongoza kongamano la Oparesheni Washa Taa Morogoro.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.