• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

MWENGE WA UHURU 2023 WAPIGA HODI MKOANI MOROGORO

Posted on: May 7th, 2023

 Mwenge wa Uhuru 2023 umeanza kukimbizwa Leo Mei 6 ukitokea Mkoani Iringa ambapo unatarajia kupitia jumla ya miradi 68 yenye thamani ya Tsh. zaidi ya Bil.12.

Ukiwa Mkoni humo Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa katika Halmashauri zote tisa ambapo leo umekamilisha mbio zake katika Halmashauri ya Mlimba iliyopo Katika Wilaya ya Kilombero.

 Ndani ya Halmashauri hiyo Mwenge wa Uhuru umepitia miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa kituo cha Afya Chita

Akizungumza na wananchi wa eneo la miradi mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa ndugu Abdallah Shaib Kaimu amesisitiza watendaji mbalimbali kukamilisha nyaraka za malipo yanayofanywa kwa mafundi zikiwemo nyaraka za ujenzi wa majengo yote ya serikali.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ndugu Abdallah Shaib Kaimu akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la mama na mtoto pamoja na upasuaji katika kituo cha Afya Chita.

Ndg. Abdallah Shaib ametoa rai hiyo wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la mama na mtoto pamoja na jengo la upasuaji.

Awali mara baada ya kuupokea  mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa amesema Mwenge utakimbizwa katika Halmashauri zote tisa za Mkoa wa Morogoro kwa umbali wa Km 1,588 na utapitia jumla ya miradi ya maendeleo ipatayo 68 yenye thamani ya Shilingi za kitanzania 12,170,922,197.46.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego baada ya kukamilisha mbio zake Mkoani Iringa.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kuwa Kati ya miradi 68 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru, miradi 5 itafunguliwa, miradi 19 itazinduliwa, miradi 20 itakuwa ya kuonwa na miradi 24 itawekewa mawe ya msingi.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa akizungumza na Viongozi na wananchi ambao wamejitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru  ukitokea Mkoani Iringa.

Miradi yote hiyo imefanikiwa kufika hapo ilipofikia kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali, Wananchi na Wadau mbalimbali  wa maendeleo.

Mradi wa madarasa matano katika Shule ya Sekondari Ngai ni miongoni mwa miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Chita Dkt. Karim Msola ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanikisha ujenzi wa Wodi ya mama na mtoto pamoja na jengo la upasuaji ambalo litaokoa maisha ya wanawake wajawazito na watoto zaidi ya 20,000 ambao walikuwa wanatembea umbali wa zaidi ya kilometa 21kufuata huduma za Afya katika vijiji vingine.

Viongozi mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Morogoro, Wakurugenzi wa Halmashauri, na Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro wameshiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.