MWENGE WA UHURU 2024 WASISITIZA UPENDO, UMOJA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII
Mwenge wa Uhuru 2024, umewataka watanzania wote hapa nchini kudumisha tunu za Taifa hili zizoazishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuendelezwa na waandamizi wake ambazo ni UPENDO, UMOJA NA AMANI.
Hayo yamebainishwa leo Aprili, 25 na Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi. Maria Mapunda wakati akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya shule ya Msingi Kiswago Wilayani Malinyi Mkoani Morogoro muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili na matundu manne ya vyoo.
Mkimbiza Mwenge Bi Mariam Mapunda amesema Amani, Upendo na Umoja ndio tunu bora zinazotakiwa kulindwa kwa kuvu zote na watanzania kwa kuwa ndio nguzo ya Taifa letu na chanzo cha amani hivyo kusaidia nchi kuendelea kukua kiuchumi.
Pamoa na kiongozi huyo kuwakumbusha watanzania kudumisha tunu hizo, bado amewakumbusha wananchi wa Wilaya ya Malinyi na watanzania wote kwa ujumla kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu isemayo TUNZA MAZINGIRA, SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA UJENZI WA TAIFA ENDELEVU
Aidha, amewakumbusha kutekeleza kaulimbiu za kupinga vita Rushwa, kupinga ugonjwa wa UKIMWI, kutokomeza ugonjwa wa malari pamoja na kujijengea tabia ya kula vyakula bora na vyenye Virutubisho ili kuondokana na magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na kutokula vyakula bora.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Malinyi umepitia miradi ya Maendeleo sita ambayo ni mradi wa kuona miche na Mazingira, kuzindua Mradi wa Maji Sofi Mission, kuona mradi wa Vijana, kuzindua ukarabati wa jengo la mionzi na kuzindua mradi wa madarasa mawili na matundu Manne ya Vyoo katika shule ya Msingi Kiswago yote kwa pamoja yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Mil. 400.
Kesho Aprili 26 ikiwa ni siku ya saba tangu Mwenge wa uhuru kuanza kukimbizwa Mkoani Morogoro, Mwenge huo utakimbizwa katika Halmashauri ya Ifakara Mji na utakuwa umebakiza halmashauri mbili tu kukamilisha halmashauri zote tisa za Mkoa huo za kukimbiza Mwenge huo
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.