Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndg. Abdallah Shaib Kaim amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwa utekelezaji mzuri na usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amepokea Mwenge wa Uhuru pamoja na viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wakitokea Wilayani kwa ajili ya kuendelea kukimbizwa katika Halmashauri hiyo.
Ndg. Shaib ametoa pongezi hizo Mei 8 mwaka huu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi katika shule ya msingi ya Itete Njiwa iliyopo Wilayani humo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 ndg. Abdallah Shaib Kaim ameongoza zoezi la upandaji miti katika enelo la shule ya Sekondari Njiwa iliyopo Wilayani Malinyi.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge amesema amejiridhisha na nyaraka mbalimbali za miradi ya maendeleo kwa kuzipitia kwa umakini ili kujiridhisha na taarifa zilizomo, ubora wake na vigezo vya mradi na kubaini kuwa miradi hiyo imekidhi vigezo vya kuwekewa jiwe la msingi, kuonwa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
“...nitumie fursa hii kuwapongeza wote, Mkuu wa Wilaya, Mbunge, viongozi wa Halmashauri, mmefanya vizuri, mradi umekidhi vigezo... hivyo Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 umeridhishwa na taarifa za mradi.
Aidha, Ndg. Shaib amewahimiza wakazi wa Itete na Tanzania kwa ujumla kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwa rushwa ni adui wa haki na wa maendeleo ya nchi hivyo hawanabudi kushikamana kupiga vita Rushwa.
Awali, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kipenyo Bi. Restuta Kumpindi akisoma taarifa ya ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Zahanati ya kijiji hicho, amesema ujenzi huo uliogharimu zaidi ya Tsh. milioni 81,389,240 utasaidia wananchi 4099 kupata huduma za matibabu katika vijiji vya jirani, kwani wakazi hao walikuwa wanatembea umbali wa kilometa tano kufuata huduma ya Afya kituo cha Afya Mtimbila.
Nae, Mbunge wa jimbo la Malinyi Mhe. Antipasi Mgungusi amempongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.
Mwenge wa Uhuru unatarajia kuendelea kukimbizwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara kesho Mei 9 mwaka huu.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.