Mwenge wa Uhuru 2024 umepongeza Wakala ya Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Morogoro kwa kutumia kikamilifu mfumo wa manunuzi kwa njia ya kidijitali yaani NeST wakzti wa kutangaza zabuni zake ndani ya Mkoa huo kama yalivyo matakwa ya Serikali.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 27, 2o24 na Kiongozi. Wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Godfrey Mnzava wakati wa kuweka jiwe la msingi barabara ya nzege ya Kichangani katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro yenye urefu wa M.400 huku ukigharimu shilingi za kitanzania 400mil.
Akisisitiza matumizi ya mfumo wa NeST, kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amsema serikali imerdhia mfumo huo utumike na Ofisi zote za Serikali, wakala wa Serikali na Mashirika yote ya Umma yanatakiwa kutumia mfumo huo ili kuondoa malalamiko kwa wazabuni waoomba tenda Serikalini huku akibainisha kuwa mfumo huo pia unatum8ka katika kudhibiti matumizi mabaya ya Serikali.
Hata hivyo kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge Kitaifa ameonekana kufurahishwa na TARURA Mkoa wa Morogoro kwa kutumia mfumo huo wakati wa kujenga barabara kwani nyaraka zote zimeonesha kutumika kwa mfumo huo wa NeST
Kuondoa adha ya wananchi wa Mtaa wa Kichangani walipokuwa wakitoka kwenda kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa kutumia barabara hiyo iliyokuwa na mashimo pamoja na tope na Serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuamua kuwaondolea wananchi adha hiyo.
Mwenge wa Uhuru leo umekimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kupitia miradi 10 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi za kitanzania. 3. 6Bbaada ya kupokea kutoka Halmashauri ya Mji Ifakara Wilaya ya Kilombero.
Kesho Aprili 28,2024 Mwenge wa Uhuru utakamilisha mbio zake Mkoani Morogoro kwa kukimbiza Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro DC.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.