Mwenge maalum wa Uhuru kwa mwaka 2021 umekamilisha mbio zake Mkoani Morogoro Agosti 10 mwaka huu, baada ya kukimbizwa Mkoani humo kwa siku saba kuanzia Agosti 4 mwaka huu ukiongozwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Luteni Josephine PaulMwambashi.
Ukiwa Mkoani Morogoro Mwenge Maalum wa Uhuru umekimbizwa umbali wa km 1,294.45 na kupitia miradi ya maendeleo 44 yenye Thamani ya zaidi ya Tsh. 9 Bil. ambayo iko katika sekta ya Afya, Elimu, Maji na Kilimo ambapo kati ya hiyo miradi miwili pekee ndiyo ambayo ilikataliwa na mwenge kwa sababu mbalimbali.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge kitaifa Luteni Josephine Mwambashi pamoja na kuwaeleza wananchi ujumbe wa Mwenge wa mwaka huu ambao ni “TEHAMA NI SMINGI WA TAIFA ENDEREVU; ITUMIE KWA USAHIHI NA UWAJIBIKAJI” amekuwa mara zote akisisitiza juu viongozi wa Umma kuwa waadilifu huku akiwataka wale waliopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maendeleo kuwa waaminifu na wazalendo kwa nchi yao.
Makabidhiano ya Mwenge wa uhuru baina ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Pwani AbubakariKunenge yamefanyika Agosti 11 mwaka huu katika viwanja vya shule ya Msingi Ubenalunch Wilayani chalinze huku wakuu hao wawili wa mikoa wakikiri makabidhiano hayo.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.