Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2023 Ndg. Abdallah Shaib Kaim amewapongeza viongozi mbalimbali Mkoani humo kwa ushirikiano, mshikamano na umoja walionao katika kuhakikisha kuwa Mkoa unapata maendeleo katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Ndg. Abdallah Shaib ametoa pongezi hizo Mei 15 mwaka huu wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Morogoro kwenda Mkoa wa Pwani baada ya kukamlisha mbio zake Mkoani humo.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amesema Mwenge wa Uhuru ulipokuwa Mkoani Morogoro umejionea kwa vitendo mshikamano wa viongozi hao wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Fatma Mwassa katika kusimamia miradi ya maendeleo ambayo Serikali inatoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi hiyo.
Aidha, Ndg. Abdallah Shaib amebainisha kuwa umoja huo wa viongozi hao wananchi wanakuwa na imani na Serikali yao inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa amewashukuru wakimbiza Mwenge wa Uhuru wakiongozwa na Ndg. Abdallah Shaib na kuhaidi kufanyia kazi maagizo, maelekezo na ushauri uliotolewa wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo Mkoani humo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge wakati akipokea Mwenge huo wa Uhuru amesema kuwa Mwenge huo utapita kuona, kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi 99 yenye thamani zaidi ya tilion 4.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.