Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndugu Godfley Mnzava ameendelea kuwakumbusha Wakala wa Serikali, mashirika ya Umma na Ofisi nyingine za Serikali kutumia mfumo wa manunuzi wa kidijitali yaani NeST.
Ndugu Mnzava ametoa maagizo hayo leo Aprili 24, 2024 Wakati anaweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Kidugalo Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, Mkoani Morogoro mradi ambao utagharimu fedha za kitanzania zaidi ya shilingi 322 Mil.
Amesema, lengo madhubuti la kukumbushana mara kwa mara kuhusu mfumo wa Nest ni kutaka wazabuni wote waingie kwenye mfumo huo, washindanishwe kwa kutumia mfumo huo na yule atakayekidhi vigezo vilivyowekwa atakuwa ameshinda kihalali zabuni hiyo hivyo mfumo huo utaondoa manung'uniko ya wazabuni.
Mradi huo ambao uko katika kata ya Iragua unajengwa tanki la maji lenye ujazo wa lita 7,5000 na unakwenda kunufaisha wananchi 6,700 na kwa sasa unatoa huduma ya maji kwa wakazi 5,814.
Lengo kuu la mradi huo ni kutatua changamoto ya Maji kwa wananchi wa kijiji cha Kidugalo wapatao 5,814 kupitia fedha zilizotokana na mfuko wa maji wa Taifa (NWF).
Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Ulanga umeweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Kidugalo, mradi ambao umejengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na fedha za ujirani mwema(CSR) kutoka Kampuni ya Kilombero Valley Teak (KVTC)
Kesho Aprili, 24, 2024 Mwenge wa uhuru wenye kaulimbiu Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo ya Taifa Endelevu, unaendelea na mbio zake katika Wilaya ya Malinyi
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.