Mwenge wa Uhuru wasisitiza ufuatiliaji, usimamizi miradi ya maendeleo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg. Abdallah Shaib Kaim amewataka Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kufuatilia na kusimamia kwa karibu miradi ya maendeleo katika maeneo yao kwa kuwa Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Ndg. Abdallah Shaib ametoa kauli hiyo Mei 10 mwaka huu kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa shule shikizi ya Mhovu iliyopo Kata ya Ruaha Wilayani Kilosa.
Kiongozi huyo wa mbio za mwenge amesema Serikali inatoa fedha nyingi kwa kila miradi ili iweze kutekelezwa na kutoa huduma kwa wananchi wake hivyo Viongozi wa maeneo husika wanatakiwa kufuatilia ili kujiridhisha na hali ya utekelezaji wake.
“…Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 unasisitiza kwa kupitia ofisi yako Mkuu wa Wilaya, Mbuge na Viongozi wa Halmashauri kufuatilia miradi hiyo kwa karibu…” amesema Ndg. Abdallah Shaib.
Akiwa katika shule ya sekondari ya Mazinyungu amewataka wote Kila mmoja mahali alipo kujijengea Tabia ya kupanda miti na kutunza ili kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo vya maji.
Awali akiwa katika mji mdogo wa Mikumi Kiongozi huyo na ujumbe wake wametembelea Hospitali ya St. Kizito iliyopo Mikumi Wilayani Kilosa kutoa pole kwa wagonjwa, na kugawa msaada wa vyakula kwa wanawake wajawazito ikiwa ni pamoja na sukali na Michele.
Kwa upande wake mbunge wa Kilosa Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Jimbo lake.
Mwenge wa Uhuru umekamilisha mbio zake Wilayani Kilosa ambapo umepitia Miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya Tsh bilioni 1.2.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.