Ni siku ya tano tangu Mwenge wa Uhuru 2024 kukimbizwa Mkoani Morogoro. Licha ya kukumbana na mabonde na milima, tope na kuvuka maji mengi, Mwenge wa Uhuru umefanikiwa kuwasili katika Halmashauri ya Ulanga, Halmashauri ya tano kati ya Halmashauri tisa za Mkoa wa Morogoro.
Ukiwa Wilayani Ulanga Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa Bustani ya Miche ya Mitiki kwa mfumo wa Kitalu nyumba (Green House). Ni mradi wa uhifadhi wa mazingira na unamilikiwa na Kampuni ya KILOMBERO VALLEY TEAK COMPANY (KVTC). Ni kampuni inayojishughulisha na uoteshaji wa miche, upandaji wa miti mashambani na uchakataji wa magogo yatokanayo na miti iliyovunwa.
Meneja wa KVTC Bw. Jeremia Gumadi anasema mti wa mtiki ni mti mgumu ambao unatumika kwa kutengenezea furniture na vyombo vya baharini kwa sababu ni mti mgumu hauozi lakini pili hauzami badala yake unaelea. Lakini pia TEAK unatumika kwa kutengenezea flemu za Milango na madirisha Pamoja na vifaa vya michezo mbalimbali.
Aidha; Bw. Gumandi amesema KVC ina hekta 28,000 kati ya hizo hekta 8,000 zimepandwa miti ya mitiki na eneo la hekta 20,000 limeachwa kwa ajili ya miti ya asili kwa ajili ya kutunza mazingira.
Mradi huu unagharimu kiasi cha shilingi 379,420,000, na unalenga kuzalisha miche 600,000 kila mwaka ambapo miche 400,000 hupandwa katika shamba la KVTC na miche 200,000 hugawiwa kwa wananchi ili wapande kwenye maeneo yao na hivyuo kutunza mazingira.
Manufaa ya mradi huu ni Pamoja na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi, kutoa kodi kwa serikali, vijiji 11 vinavyopakana na kampuni ya KVTC vinapata mrahaba Pamoja na kutoa ajira ya wananchi 700 inyowazunguka.
Kabla ya Mwenge wa uhuru 2024 kuzindua mradi huo, ujumbe mwenge ulitolewa kwa wananchi na msisitizo mkubwa ulikuwa ni kutunza mazingira kama ilivyo kwenye ujumbe wa Mwenge, Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa Serilikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu.
Ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, Mwenge wa Uhuru 2024 utatembelea miradi 8 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 2.9 Bil. ukitembea na kaulimbiu ya UHIFADHI WA MAZINGIRA NA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.
Kesho Aprili, 25,2024 mwenge wa uhuru utakimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.